BENKI YA NMB YAJA NA MASTA BODA KUWAWEZESHA BODABODA NCHINI - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Wednesday, 16 October 2019

BENKI YA NMB YAJA NA MASTA BODA KUWAWEZESHA BODABODA NCHINI

Mwendesha Bodaboda, Masoud Seif akiwa ampempakia Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Jenista Mhagama wakati wa uzinduzi wa huduma ya NMB MASTA BODA iliyozindulia jijini Dar es Salaam. katikati ni Kaimu Mkurugenzi wa NMB, Ruth Zaipuna na kushoto ni Mrakibu wa Polisi Abel Swai.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Jenista Mhagama akizungumza alipokuwa akizinduwa huduma ya NMB MASTA BODA iliyozindulia jijini Dar es Salaam kuwawezesha waendesha bodaboda nchini.

Kaimu Mkurugenzi wa NMB, Ruth Zaipuna akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa huduma ya NMB MASTA BODA iliyozindulia jijini Dar es Salaam na Benki ya NMB kuwawezesha waendesha bodaboda.

Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi, Biashara ndogo na za Kati wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa huduma ya NMB MASTA BODA iliyozindulia jijini Dar es Salaam na Benki ya NMB kuwawezesha waendesha bodaboda.

Huduma mbalimbali zikitolewa kwenye hafla ya uzinduzi huo.

Huduma mbalimbali zikitolewa kwenye hafla ya uzinduzi huo.


BENKI ya NMB imezinduwa huduma mpya ya NMB MASTA BODA ambayo inawawezesha madere wa pikipiki za abiria maarufu kama bodaboda kuendesha shughuli zao huku wakijiwekea akiba benki moja kwa moja kutoka kwa mteja wake.

Huduma hiyo imezinduliwa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Jenista Mhagama huku akiwataka 'bodaboda' kutumia fursa hiyo vema.

Katika huduma hiyo inamwezesha abiria wa bodaboda kufanya malipo ya nauli kwa kutumia simu za mkononi na fedha kwenda moja kwa moja kwenye akaunti ya NMB ya dereva wa bodaboda.

Akizungumza Bi. Mhagama alisema Serikali inatambua huduma inayotolewa na kundi la bodaboda hivyo kuwataka kundi hilo sasa kujihusisha na taasisi rasmi kama Benki ya NMB ili kuendelea kujenga mahusiano mazuri kibiashara.

Aida alibainisha kuwa sekta hiyo kwa sasa inatambulika na kuheshimika  hivyo kuwataka kundi hilo kutambua kuwa linamchango mkubwa kiuchumi.

No comments:

Post a Comment