Na Prisca Ulomi, Kigoma
NAIBU Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye amesema kuwa mwananchi hataweza kupiga wala kupigiwa simu kama hajasajili laini ya simu yake ya mkononi kwa alama za vidole ifikapo tarehe 31 Desemba, 2019
Nditiye ameyasema hayo akiwa kwenye ziara yake ya kikazi Mkoani Kigoma kwenye wakati akihamasisha na kuelimisha wananchi wa Kata ya Ruhita, Kibuye, Mrufiti, Itaba, Murungu, Rugongwe, Kasulu na Kibondo mjini umuhimu wa kusajili laini zao za simu za mkononi
“Serikali imeamua watanzania wote wasajili laini zao za simu za mkononi kwa kutumia alama za vidole ili kila anayepiga simu au kupigiwa atambulike ili kupunguza changamoto zinazojitokeza ili mawasiliano yaweze kuchangia kikamilifu uchumi wa chi yetu,” amesema Nditiye.
Amefafanua kuwa Sekta ya Mawasiliano imeshika nafasi ya tatu kwa mwaka 2016/2017 na ya nne kwa mwaka 2017/18 kwa kuchangia pato la taifa kwa kiwango cha asilimia 13.1 na kuwa kati ya Sekta tano bora zinazochangia pato la taifa. Serikali ieamua kusimamia kikamiifu Sekta hii ili kuhakikisha kuwa inadhibiti wizi wa mtandaoni kupitia simu za mkononi, ulaghai, uchochezi, utapeli a matumizi mengine ya simu za mkononi kwa kuwa kila mwanachi atakuwa amesajili laini yake ya simu ya mkononi kwa alama ya kidole.
Amewahamasisha wananchi waishio maeneo mbali mbali mkoani humo wakati alipofanya nao mkutano wa hadhara kuwa kuanzia mwezi Oktoba mwaka huu, wataalamu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania wakiambatana na kampuni za simu za mkononi, Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa, Jeshi la Polisi na Uhamiaji watafika maeneo mbali mbali mkoani humo ili kuendesha zoezi la kusajili laini za simu kwa wananchi wote wanaotumia na kumiliki simu za mkononi.
Amesema kuwa zoezi hili litafanyika kwa umakini mkubwa ili kuhakikisha kuwa watanzania halali wanaotambulika na wenye kadi ya NIDA au namba ya utambulisho kutoka NIDA wanasajili laii zao ili kuepusha kufanya usajili kwa watu wasiohusika kwa kuwa mkoa wa Kigoma uko mpakani ambapo kuna mwingiliano wa watu kutoka nchi za jirani
Naye Japhet Amos, mkazi wa kijiji cha Kigina kilichopo kata ya Rugongwe, Kigoma akizungumza kwa niaba ya wananchi wenzake alimuomba Nditiye kuhakikisha kuwa wananchi wanapata kitambulisho cha NIDA au namba ya utambulisho kwa wakati ili wasizimiwe simu zao mara baada ya tarehe ya wisho iliyowekwa na Serikali kufika a kuomba huduma hiyo ya usajili itolewe bure.
Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, Kanda ya Kati, Antonio Manyanda aliwafahamisha na kuwatoa hofu wananchi wote nchi nzima kuwa huduma ya kusajili laini ya simu ya mkononi kwa alama ya kidole ni bure na hakuna mwananchi yeyote atakayelazimika kulipia gharama hiyo na ametoa wito kwa wananchi kuiarifu TCRA yenye ofisi zake sehemu mbali mbali nchini kuhusu jambo hilo endapo mwananchi yeyote atatozwa gharama za kusajili laini yake na wakala wa kampui yeyote ya simu
“Usajili wa laini ya simu kwa alama ya vidole ni bure nchi nzima, mwananchi haruhusiwi kulipa gharama yeyote kwa ajili ya kusajili laini ya simu,” amesisitiza Manyanda
Katika hatua nyingine, akiwa ziarani mkoani humo, Nditiye amekagua upatikanaji wa mawasiliano kwenye kata ya Kibuye, Murungu, Rugongwe na Itaba na kutembelea minara inayotoa mawasiliano kwa wananchi waishio maeneo hayo na kubaini uwepo wa mawasiliano wakati wa asubuhi na jioni na kufifia au kukosekana kabisa wakati wa usiku ambapo ameiagiza UCSAF kwa kushirikiaa na TCRA na kampuni za simu zenye minara yake maeneo hayo kuongeza betri za kutosha ili kuapata umeme wa jua wa kuendesha minara hiyo kwa lengo la kuwawezesha wananchi kupata huduma za mawasiliano hata nyakati za usiku.
“Mawasiliano yako chini sana, mtu anapatikana kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa kumi na moja jioni, matukio yanatokea usiku hatuna msaada na tuna mtandao mmoja tu wa Vodacom,” amesema Emil Mfanye, Diwani wa Kata ya Murungu akizungumza kwa niaba ya wananchi kwenye mkutano wa hadhara wa Nditiye na wakazi wa kijiji cha Kumhasha alipokuwa kwenye ziara yake mkoani humo ya kukagua upatikanaji wa huduma za mawasiliano, kuhamasisha wananchi kusajili laini za simu kwa alama ya vidole na kutoa elimu ya manufaa ya anwani za makazi na postikodi
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
No comments:
Post a Comment