Mkufunzi kutoka Mradi wa Boresha Habari ukiendeshwa chini ya uratibu wa mashirika yasiyo ya Kiserikali ya Internews na FHI 360 unaofadhiliwa na Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID),Temigunga Mahondo akiwaeleza waandishi wa habari wa kituo cha redio Nuru Fm Iringa juu ya kusaidia kupaza sauti za wanyonge kupitia kalamu zao, hususani wale ambao wanaishi maeneo ya vijijini.
Baadhi ya waandishi wa habari wa kituo cha redio Nuru Fm Iringa wakimsikiliza mkufunzi kutoka Mradi wa Boresha Habari ukiendeshwa chini ya uratibu wa mashirika yasiyo ya Kiserikali ya Internews na FHI 360 unaofadhiliwa na Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID),Temigunga Mahondo wakati akitoa elimu kwa juu ya kusaidia kupaza sauti za wanyonge kupitia kalamu zao, hususani wale ambao wanaishi maeneo ya vijijini.
NA FREDY
MGUNDA, IRINGA
WAANDISHI wa
habari wa Kituo cha Redio, Nuru FM 93.5 mkoani Iringa wametakiwa kujikita
kuandika habari za uchunguzi kwa kuibua matatizo ndani ya jamii, ambayo
yamekuwa yakifichika na kutopaziwa sauti, jambo ambalo litawasaidia wananchi
kutatulia kero ambazo zimekuwa zikiwakabili sababu ya kukosa sehemu pa
kuzisemea.
Hayo yamebainishwa na mkufunzi kutoka Mradi wa Boresha Habari ukiendeshwa chini ya uratibu wa mashirika yasiyo ya Kiserikali ya Internews na FHI 360 unaofadhiliwa na Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID),Temigunga Mahondo wakati akitoa elimu kwa waandishi wa habari wa kituo cha redio Nuru Fm Iringa juu ya kusaidia kupaza sauti za wanyonge kupitia kalamu zao, hususani wale ambao wanaishi maeneo ya vijijini.
Alisema waandishi wa habari wanamsaada mkubwa sana ndani ya jamii kwa kupaza sauti za wanyonge kupitia kalamu zao, kwa kuibua matatizo ambayo yamekuwa yakiwakabili wananchi, na hasa kwa kuandika habari za uchunguzi ili jamii ipate kutatuliwa kero zao.
“Naombeni waandishi wa habari mjikite zaidi kuandika habari za uchunguzi kwa kuibua matatizo ambayo yamekuwa yakijificha ndani ya jamii, hususani kwa wale wananchi wanaoishi maeneo ya vijijini, ambao wamekuwa wakikosa wa kuwapazia sauti na kuendelea kuishi maisha ya shida,”Alisema Mahondo
Mahondo alisema kuwa
waandishi wa habari mkijikita kwenye habari hizi mtakuwa mnaisaidia jamii ya
wananchi wale wale wanyonge kwa kuwa tayari mtakuwa ninyi ndio sauti yao kwa
kipindi chote ambacho mtakuwa mnaandika habari hiz.
“Kuandika habari hizi
zinanafasisi kubwa wa kuzifanya kwa kuangalia changamoto na manufaa katika
sekta ya Afya,sekta elimu,sekta ya miundombi,sekta ya kilimo na mazingira na utapata uwanda mpana sana wa kufanya habari
zenye tija kwa jamii” alisema Mahondo
Aidha Mahondo alisema,licha
ya jamii kuhitaji kupata habari za kiburudani ambazo zimekuwa zikiwaburudisha
kwa muda mfupi tu lakini kubwa zile habari ambazo zinasaidia kutatua changamoto
za wananchi ndio zinatija hasa kwenye jamii kwa kufanikisha kutatua matatizo
yao.
“Hakuna wananchi ambaye hapendi kupata burudani hivyo
tunaangalia aina gani ya burudani ambayo inawapa zaidi furaha jamii kwa kipindi
kirefu ambayo itawasaidia kufanya shughuli za kimaendeleo ambazo zitawaletea
faida wananchi” alisema Mahondo
Naye mwaandishi
wa habari na mtangazaji wa kipindi cha
Sunrise Power cha Nuru fm Godfrey Mengele aliwatupia lawama wananchi hususani
wa maeneo ya vijijini, ambapo wamekuwa waoga kutoa ushirikiano kwa waandishi wa
habari kwa kushindwa kuzungumza matatizo yanayowakabili.
alisema kuwa waandishi wa habari hawezi kuchunguza habari bila ya kupewa taarifa (Tipu) juu ya tatizo linalo wakabili wananchi, pamoja na kutozungumza na wahusika waliofanyiwa matukio hayo ya ukatili ama ndugu, ambapo wananchi hao hua hawapo tayari kuzungumza na kuwakimbia waandishi.
Mengele aliwataka wananchi kuachana na tabia za uoga pale wanapotaka kusemewa matatizo yanayo wakabili kupitia vyombo vya habari, bali wawe karibu na media ambazo ndio msaada mkubwa kwao.
“Wananchi wamekuwa
waoga sana kutupa habari ambazo zinawagusa wao kwa kuhofia kufikishwa polisi,kwenye
ofisi za serikali za mitaa hata mahakamani kutoa ushaidi ndio maana waandishi
tunapata wakati mgumu pia kuandika habari hizi” alisema Mengele
Lakini alitoa
rai kwa waandishi wa habari kujikita kuandika habari za kichunguzi ambazo ndio
zimekuwa zikiibua matatizo ya wananchi na kutafutia ufumbuzi wa kutatua
changamoto zao.
Kwa upande
wake mtangazaji wa kipindi Street Bamiza Roger Magoha alisema mafunzo aliyopata
yatamsaidia kukuza vipaji halisi vya wasanii wanaopenda kutoa burudani na kujua
aina gani ya burudani wasikilizaji wanapenda kusikiliza.
“Sasa nitafanya
uchunguzi kujua wasikilizaji wangu wanapenda aina gani ya burudani kwa kuwa
nimeshapata mbinu za kufanya uchuzi huo kutoka kwa mkufunzi wa Mradi wa Boresha
Habari ukiendeshwa chini ya uratibu wa mashirika yasiyo ya Kiserikali
ya Internews na FHI 360 unaofadhiliwa na Shirika la Marekani la Maendeleo ya
Kimataifa (USAID),Temigunga Mahondo” alisema Magoha
Magoha aliongeza kwa
kusema kuwa amejifunza kufanya mahojiano bora na wasanii mbalimbali pamoja na
viongozi hivyo mafunzo hayo yamemwogezea kitu kipya kichwani mwake ambacho hapo
awali hakuwa nacho.
Tarehe 17
Januari 2018, Serikali ya Marekani kwa kupitia Shirika la Marekani la Maendeleo
ya Kimataifa (USAID), ilizindua mradi wa kuimarisha asasi za kiraia na
vyombo vya habari uitwao Boresha Habari Katika hafla fupi
iliyofanyika jijini Dar es Salaam, mradi huo ukiendeshwa chini ya uratibu wa
mashirika yasiyo ya Kiserikali ya Internews na FHI 360, mradi wa Boresha
Habari utashirikiana na wabia wa Kitanzania, ikiwa ni pamoja na: Baraza la
Habari Tanzania, Tanzania Bora Initiative, na Jamii Media; ili kuboresha weledi
miongoni mwa waandishi wa habari na kusaidia kuweka mazingira yaliyo wazi kwa
vyombo vya habari.
“Serikali ya
Marekani imedhamiria kwa dhati kusaidia kuinua ujuzi na weledi wa vyombo vya
habari na asasi zisizo za kiserikali za Kitanzania hususan katika kuwawezesha wanawake na vijana
kupaza sauti zao na kueleza dukuduku zao kwa ufanisi,”
Katika kipindi cha miaka mitano ijayo, mradi
wa Boresha Habari unalenga kufanya kazi na wadau wa vyombo vya
habari katika mikoa ya Dar es Salaam, Zanzibar, Iringa, Mbeya, Morogoro,
Arusha, Manyara, Dodoma, Tanga, Mtwara, Mwanza na Kigoma.
Aidha, mradi
wa Boresha Habari utatoa mafunzo na msaada wa kitaalamu kwa vyombo vya habari
vya humu nchini ukivisaidia kuanza kutumia teknolojia za kidijitali na
kuimarisha uwezo wao wa kiusimamizi na kifedha.
Hali kadhalika, mradi huu
utatoa mafunzo kwa asasi za kiraia ili ziweze kushirikiana vyema na vyombo vya
habari katika kusukuma mbele jitihada zao. Kwa kuzingatia umuhimu wa redio za
jamii kama vyanzo maarufu vya habari za maeneo husika, mradi wa Boresha
Habari utafanya kazi na vituo mbalimbali vya redio nchini kote ili
kuboresha uwezo wao wa kitaalamu na uendelevu katika masuala ya kifedha.
No comments:
Post a Comment