MINADA YA MIFUGO RUKWA YAINGIZA BILIONI 18.8 KWA WAFUGAJI - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Friday 26 April 2019

MINADA YA MIFUGO RUKWA YAINGIZA BILIONI 18.8 KWA WAFUGAJI

Mkuu wa mkoa wa Rukwa mh. Joachim Wangabo (kushoto) akipokea cheti cha pongezi kwa kusimamia utekelezaji wa Ilani ya CCM katika Mkoa wa Rukwa kutoka kwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Reiner Lukala (kulia).

MKUU wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo ameendelea kuwasisitiza wafugaji kuendelea kufuga kisasa baada ya biashara ya mifugo katika minada ya awali na ule wa mpakani na nchi ya Zambia katika Kijiji cha Kasesya kuwaingizia wafugaji hao shilingi 18,890,665,000 kutokana na kuuza ng’ombe 35,532, mbuzi 2,307 na kondoo 631.
Ameyasema hayo alipokuwa akiwasilisha utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kwenye kiako cha Kamati ya Siasa ya Mkoa kwa kipindi cha mwezi July hadi Disemba, 2018 na kuhudhuriwa na wataalamu kutoka Halmashauri, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa pamoja na wakuu wa Taasisi na Mamlaka za Serikali zilizopo katika Mkoa.
Aidha, amepongeza ongezeko la makusanyo yay a vibali vya kusafirishia mifugo kwa silimia 33.6 kwa mwaka wa fedha 2018/2019, mafanikio ambayo yametokana na udhibiti wa pamoja wa Uongozi wa Mkoa pamoja na Wizara ya Mifugo na Uvuvi.
“Mapato ya Serikali Kuu yanayotarajiwa kukusanywa kwa Mwaka wa Fedha 2018/ 2019 kutokana na ushuru wa vibali vya kusafirisha Mifugo ni Shilingi 80,000,000/=. Hadi kufikia tarehe 31 Desemba, 2018 Mapato ya Serikali Kuu yaliyopatikana kutokana na ushuru wa vibali vya kusafirisha Mifugo ni Shilingi 120, 44,500/=.  Makusanyo hayo ni zaidi ya Shilingi 40,444,500/= ya lengo la Mwaka,”Alisema.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Rukwa Reiner Lukala amewapongeza wataalamu wanaoendelea kuitekeleza Ilani ya CCM kwa umakini pamoja na ushirikiano wanaoutoa katika kupokea ushauri na kuufanyia kazi pale inapostahili.
“Kwa wataalamu nichukue fursa hii kuwashukuru kwa jinsi mnavyotumia wakati wenu, elimu yenu, ujuzi wenu na muda wenu kwa kuendelea kufanya kazi kubwa ya utekelezaji wa Ilani, Sura ya 8 ya Ilani ya CCM ya Mwaka 2015 inatuelekeza sisi Chama cha Mapinduzi kuwasimamia ninyi kuona mnafanya nini, lakini kwa niaba ya CCM nichukue fursa hii kuwapongeza sana kwamba mpaka wakati huu tunaenda vizuri,” Alisema.
Katika kikao hicho cha kuwasilisha utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi Mkuu wa mkoa wa Rukwa alipewa cheti cha kutambuliwa juhudi zake za kuhakikisha anatekeleza ilani hiyo hatua kwa hatua na kwa wakati kupitia ofisi yake ya Mkoa pamoja na kuzisimamia kikamilifu halmashauri nne za mkoa huo.

No comments:

Post a Comment