KRISMASI, ITUKUMBUSHE KUILINDA UHAI - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Sunday, 28 December 2025

KRISMASI, ITUKUMBUSHE KUILINDA UHAI

Mkurugenzi wa Human Life International (HLI) Kanda ya Afrika' Kwa Nchi Zinazozungumza Kiingereza, EMIL HAGAMU.

KATIKA ujumbe wake wa sikukuu ya Kuzaliwa kwa Yesu Kristo, Mkurugenzi wa Shirika la Kutetea Uhai Tanzania (Pro-Life), Emily Hagamu, amewakumbusha waamini wa Kikristo kuwa kuzaliwa Kristo ni ukumbusho kwa jamii kuthamini uhai wa kila binadamu.


“Kuzaliwa kwa Yesu Kristo kunatukumbusha kuwa kila uhai una thamani kubwa mbele za Mungu, hivyo ni wajibu wa kila mtu kuilinda na kuithamini maisha ya binadamu katika hatua zote za uhai,” alisema Hagamu.


Ameongeza kuwa jamii inapaswa kutumia kipindi cha sikukuu kuimarisha maadili ya upendo, huruma na mshikamano, hususan kwa watoto, wajawazito na makundi yaliyo hatarini dhidi ya vita vya Watu wanaondeleza utamaduni wa kifo, na nia ovuo katika maadili ya Watanzania.

“Tunaposherehekea Krismasi, tuchague kusimama upande wa uhai, kuunga mkono familia na kulea kizazi chenye heshima kwa maisha,” amesisitiza, akihimiza ushiriki wa pamoja katika kulinda na kutetea uhai nchini Tanzania.

Amesema kama vile ambavyo kuzaliwa kwake Kristu ni furaha kwa Ulimwengu, basi hata jamii haina budi kufurahi kuzaliwa Mtoto katika familia kwani kila mzaliwa mpya katika familia huleta baraka yake.

No comments:

Post a Comment