KAMPUNI YA HAFFIYY ENTERTAINMENT MKOMBOZI KWA WASANII BONGO FLEVA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Friday 26 April 2019

KAMPUNI YA HAFFIYY ENTERTAINMENT MKOMBOZI KWA WASANII BONGO FLEVA

 Mkurugenzi wa kampuni ya Haffiyy entertainment Hafidh Mkongwa akiongea na waandishi wa habari juu ya mikakati ya kampuni hiyo kuinua vipaji na kuirudhisha Iringa kwenye ramani ya burudani.


NA FREDY MGUNDA, IRINGA

KAMPUNI ya Haffiyy entertainment  ya mkoani Iringa imejipanga kuhakikisha inainua vipaji vya wasanii wa bongo fleva mkoani Iringa kwa lengo la kuwakomboa vijana kuirudisha Iringa kwenye ramani ya Muziki kama ilivyokuwa hapo awali.

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Iringa mkurugenzi wa kampuni ya Haffiyy entertainment Hafidh Mkongwa alisema kuwa lengo la kampuni hiyo ni kuhakikisha wanakuza vipaji vya wasanii wa bongo flava kwa kuongeza ajira kwa vijana.

“Kuna wasanii wengi wanavipaji lakini wanakosa wasimamizi wazuri hivyo kampuni yangu imejipanga kuhakikisha inawasimamia vilivyo kwenye sanaa hii na kuwaongezea kipato lakini kukuza pia vipaji vyao” alisema Mkongwa

Mkongwa alisema kuwa mkoa wa Iringa umepotea kwenye ramani ya burudani kwa muda mrefu hivyo kmapuni hiyo imeweka mikakati madhubuti kuhakikisha kuwa Iringa inarudi kwenye ramani ya burudani.

“Miaka ya nyuma Iringa ilikuwa kwenye ramani ya burudani na ilikuwa inazalisha vipaji vingi hivyo hapa katika tumepotea kwenye ramani hiyo hivyo kamapuni yangu imejipanga vilivyo kuhakikisha wasaniii wa mkoa wa Iringa wanarudi kwenye ramani ya burudani” alisema Mkongwa

Mkongwa alisema kwa sasa kampuni ya Haffiyy Entertainmet imeanza kuwasimamia baadhi ya wasanii kutoka mkoani Iringa na nyanda za juu kusini na sasa wameanza kumsimamia msanii aitwaye Meda Classic na msanii aitwaye Casso anatoka katika wilaya ya Temeke

“Hawa ndio baadhi tu ya wasanii ambao tumeingia nao mikataba ya kusimamia kazi zao lakini bado nawasaidia wasanii wengi ambao bado hawana mikataba na kampuni yangu hivyo mtaona jitihada zangu zimeanza kwa kasi kubwa” alisema Mkongwa

Aidha Mkongwa aliwaomba wananchi na wadau wa burudani mkoani Iringa kuendelea kuwaunga mkono kwa juhudi ambazo zinazofanywa na kampuni hiyo ili kukuza burudani na kuirudisha Iringa kwenye Ramani ya burudani.

“Iringa tulikuwa tunafanya kazi vizuri mno hivyo baada ya kupotea kwenye ramani niwaombe wadau tushirikiane kuhakikisha tunarudi kwenye ramani ya burudani” alisema Mkongwa

Mkongwa alimalizia kwa kuwaomba wasanii wenye vipaji na nidhamu ya kazi basi wamtafute ili kuhakikisha kuwa wanapata nafasi kwenye kampuni hiyo yenye leongo la kuinua vipaji vyao na kuwaongezea ajira vijana hao.

No comments:

Post a Comment