MATUKIO ZIARA YA RAIS MAGUFULI MKOANI MTWARA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Thursday, 4 April 2019

MATUKIO ZIARA YA RAIS MAGUFULI MKOANI MTWARA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiweka jiwa la msingi kuashiria ukarabati wa majengo ya Chuo cha Ualimu Kitangali kilichopo Newala Vijijini akiwa na  Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichaki, Balozi wa Canada nchini Mhe. Pamela O'Donnell na viongozi wengine Jumatano Aprili 3, 2019. Mradi wa ukarabati wa chuo hicho ni moja ya miradi inayohusisha ukarabati wa vyuo vya ualimu nchini vikiwemo vya Ndala, Shinyanga na Mpuguso kwa gharama ya shilingi bilioni 36.475 ikiwa ni ufadhili wa serikali ya Canada iliyotoa shilingi bilioni 28.275 wakati serikli ya
Tanzania imetoa shilingi bilioni 8.200.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na viongozi wa ngazi mbalimbali wa Chama cha Mapinduzi wa mkoa wa Mtwara alipopita makao makuu ya mkoa ya chama hicho ili kuwasalimia akiwa njiani kuelekea kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa barabara ya lami ya Mtwara-Newala  na ukarabati wa Chuo cha Ualimu Kitangali kilichopo Newala Vijijini Jumatano Aprili 3, 2019.

ais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na viongozi wa ngazi mbalimbali wa Chama cha Mapinduzi wa mkoa wa Mtwara alipopita makao makuu ya mkoa ya chama hicho ili kuwasalimia akiwa njiani kuelekea kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa barabara ya lami ya Mtwara-Newala  na ukarabati wa Chuo cha Ualimu Kitangali kilichopo Newala Vijijini Jumatano Aprili 3, 2019.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia maandalizi ya kubangua korosho katika kiwanda cha Yalin Cashewnut Company Ltd kilichopo eneo la Msijute Mtwara Vijijini akiwa na Waziri wa Kilimo na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa akiwa katika ziara ya kikazi ya mkoa wa Mtwara.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na wana kwaya wa Chuo cha Utumishi cha Mtwara alipowasili katika kijiji cha Naliendele kuweka jiwe la msingi katika ujenzi  wa
barabara ya lami ya Mtwara-Newala yenye urefu wa kilometa 50  ikiwa ni sehemu ya barabara ya Mtwara-Newala-Masasi yenye urefu wa kilometa 210 ambayo ikikamilika itapunguza urefu wa barabara ya ukanda wa maendeleo wa Mtwara kutoka kilometa 1,020 hadi kilometa 825.

No comments:

Post a Comment