DK MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA CHUO CHA KITANGALI NEWALA, MTWARA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Thursday, 4 April 2019

DK MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA CHUO CHA KITANGALI NEWALA, MTWARA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Balozi wa Canada Nchini Mheshimiwa Pamela O Donnell pamoja na Waziri wa Elimu  Profesa Joyce Ndalichako kabla ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa chuo cha Kitangali kinachojengwa na Serikali kwa kushirikiana na Canada Wilayani Newala Mkoa wa Mtwara. Aprili 3, 2019.

Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akiwasalimia Wananchi wa Tandahimba Mkoani Mtwara mara baada ya Msafara wa Rais wa Jamhuri Dkt. John Pombe Magufuli kusimama kwaajili ya kuwasalimia alipokuwa akielekea Kuweka jiwe la msingi la ujenzi katika chuo cha Ualimu cha Kitangali Wilayani Newala Mkoa wa Mtwara. Aprili 3, 2019.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wananchi wa Newala Mkoani Mtwara aliposimama kuwasalimia akiwa njiani kuelekea katika chuo cha Ualimu Kitangali kilichopo Wilaya ya Newala Mkoa wa Mtwara ikiwa ni muendelezo wa Ziara yake ya siku tatu Mkoani humo. 

Sehemu ya Majengo ya mapya ya Chuo cha Kitangali ambayo Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa chuo  hicho.

Sehemu ya Nyumba za makazi Mapya ya Walimu wa Chuo cha Kitangali ambayo Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa chuo  hicho. PICHA ZOTE NA IKULU.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Tandahimba wakati akiwa njiani kuelekea Masasi mkoani Mtwara. 

No comments:

Post a Comment