Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mbio hizo za Mwenge Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Jenister Mhagama ameipongeza Benki ya NMB kwa kutokana na ushirikiano wao ulichangia kufanikisha maadhimisho hayo.
Waziri Mhagama amesema kuwa, Benki hiyo imesaidia kwa sehemu kubwa kufanikisha maadhimisho hayo kwa vijana wa Halaiki.
Kwa upande wake Msimamizi wa Mahusiano ya Benki ya NMB na Serikali Vicky Bishubo alisema kuwa Benki hiyo imejiwekea utaratibu kwa kila mwaka kudhamini uzinduzi na ufungaji wa wa mbio za Mwenge Kitaifa.
‘’Tumeshiriki kwenye uzinduzi hapa mkoani Songwe, lakini pia tutashiriki wakati wa kilele cha mbio za Mwenge huko mkoani Lindi,’’ alisema Bishubo.
Amefafanua kuwa Benki hiyo imeona ni wajibu wao kushirikiana na serikali katika mambo mbalimbali na kuwa kwenye uzinduzi huo, Benki hiyo imechangia sare 800 (Traksuit) kwa ajili ya halaiki zenye thamani ya Shilingi Milioni 19.
Mbio za Mwenge wa Uhuru zimezinduliwa rasmi April 2 mkoani Songwe na zinatarajia kutumia siku 195 na kuzimwa katika mkoa wa Lindi Octoba 19 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment