MATUKIO PICHA SIKU YA USALAMA NA AFYA MAHALI PA KAZI, MBEYA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Monday 29 April 2019

MATUKIO PICHA SIKU YA USALAMA NA AFYA MAHALI PA KAZI, MBEYA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akiwa pamoja na Naibu wake Mhe.Anthony Mavunde (wa kwanza kulia) na wa kwanza kushoto ni katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Bw. Andrew Massawe wakitembea katika viwanja vya Bustani ya Jiji wakati wa kukagua mabanda ya maonesho katika kuadhimisha Siku ya Usalama na Afya Mahali Pa Kazi Aprili 28, 2019 yaliyofanyika Kitaifa Mkoani Mbeya.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akipokelewa na watumishi wa OSHA alipowasili katika viwanja vya bustani ya Jiji Mkoani Mbeya kwa ajili ya maadhimisho ya sherehe Usalama na Afya Mahali Pa Kazi yaliyofanyika mkoani hapo kitaifa.

Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Afya na Usalama Mahala Pa Kazi Bi. Khadija Mwenda akieleza jambo kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama wakati wa maaadhimisho hayo, wa kwanza kushoto ni Naibu wake Mhe. Anthony Mavunde.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akiuliza jambo kwa wataalam kutoka Idara ya Kazi wa ofisi hiyo alipotembelea banda lao wakati wa maadhimisho ya Usalama na Afya Mahali Pa Kazi yaliyofanyika Jijini Mbeya.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Wenye Ulemavu) Mhe. Stella Ikupa akiweka sahihi kwenye kitabu cha wageni katika banda la maonesho la Wakala wa Afya na Usalama mahala pa Kazi (OSHA) wakati wa maadhimisho hayo.

No comments:

Post a Comment