Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Prof. Mussa Assad. |
1.
CAG Assad: Majengo ya ofisi za CUF yamesajiliwa kwa majina ya watu badala ya
Bodi ya Wadhamini.
2.
CAG Assad: Tumebaini CCM haijawasilisha NSSF makato ya Sh. bilioni 3.74 ya
wanachama wake
3.
CAG Assad: Tumebaini Chadema ilinunua gari jipya aina ya Nisan Patrol kwa Sh
milioni 147.5 lakini lililisajiliwa kwa jina la mwanachama badala ya Bodi ya
Wadhamini.
4.
Prof Assad: Jeshi la Polisi lilipa Sh. milioni 600 kwa ajili ya mafunzo ambayo
hayakufanyika.
5.
Prof Assad: NEC ilinunua BVR 8,000 lakini mashine 5,000 kati ya hizo zilikuwa
haziendani na mfumo uliotakiwa hivyo kuisababisha serikali hasara ya mamilioni
ya shilingi
6.
Prof Assad: Pia tumebaini Wilaya ya Hanang' haikuwasilisha vitabu vya fedha na
kuna upotevu wa mapato ya Sh. bilioni 1.4 na walilipa fedha kwa wakandarasi kwa
kazi ya dharura pasipo kuwapo kwa kazi ya dharura.
7.
CAG Assad: Tumebaini kuwapo kwa malipo hewa ya mabilioni ya shilingi katika
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya
8.
Prof Assad: Serikali kuu kulikuwa na mapendekezo 91, mawili tu ndiyo
yametekelezwa kikamilifu.
9.
Prof Assad: Mapendekezo yetu tuliyotoa katika ripoti iliyopita yalikuwa 350
lakini ni 80 tu yaliyotekelezwa
kikamilifu.
10.
CAG Assad: Kuna miradi 27 serikali za mitaa imekamilika lakini haitumiki licha
ya kugharimu mabilioni ya shilingi.
11.
Prof Assad: Jeshi la Polisi lililipa Sh. bilioni 16 kwa ajili ya ununuzi wa
sare za polisi bila kuwapo kwa ushahidi wa ununuzi.
12.
Prof Assad: Kuna mafunzo kwa maofisa wa NEC hayakufanyika licha ya mzabuni
kulipwa.
Vyama vilivyofanya matumizi bila ya kuwa na nyaraka toshelezi |
No comments:
Post a Comment