KAMPUNI ya Mawasiliano ya simu ya Halotel, imeendelea kuongeza thamani na ubunifu katika mawasiliano kwa kuzindua huduma mpya iliyoboreshwa ili kuwawezesha wateja wake nchi nzima kufurahia mawasiliano wakiwa mtandao wa Halotel pekee.
Huduma hiyo mpya iendayo kwa jina la TOMATO PLUS itamuwezesha mteja wa Halotel kuongea kwa dakika 5 za mwanzo bure mitandao yote kwa kila simu atakayopiga pale atakapojiunga na huduma ya Tomato Plus.
Akiongea na waandishi wa Habari wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo, Mkuu wa kitengo cha Mawasiiano wa Halotel, Mhina Semwenda, amesema huduma hii ni ya wateja wote wa Halotel na Mteja akijiunga na huduma ya Tomato Plus, anaweza kuongea kwa dakika tano za mwanzo bure mitandao yote kwa kila simu atakayopiga.
“Huduma hii imeboreshwa zaidi kwa kuzingatia mahitaji ya wateja wetu katika mawasiliano ili kuwawezesha kuwasiliana bila kikomo kwa kupiga simu mitandao yote na kuongea kwa dakika 5 za mwanzo bure kwa kila simu watakayopiga” alisema Semwenda.
“Mteja wa Halotel anaweza kujiunga na kufurahia huduma hii kwa kupitia menu yetu ya kwaida ya *148*66# na kasha atachagua namba namba 8 ambapo ataweza kujiunga kwa siku, wiki au mwezi na kufuraha huduma ya Tomao Plus wakati wowote na mahali popote.” Alisema na kuongeza Semwenda.
Huduma ya TOMATO PLUS imelenga katika kuongeza ufanisi, nafasi na uwezo wa mawasiliano kwa wateja wa Halotel na kwa watanzania wote, wakiwemo wafanya biashara, wafanyakazi wa sekta binafsi na serikali na wateja wengine walioko sekta zingine mijini na vijijini ambako maeneo haya kwa kiasi kikubwa hutegemea njia ya simu za mkononi kuweza kuwasiliana na kupata taarifa mbali mbali kwa uhakika.
No comments:
Post a Comment