BENKI ya NMB imezindua tawi jipya wilaya ya Mbogwe mkoani Geita kwa lengo la kukidhi mahitaji ya huduma za kifedha kwa wateja hivyo kusaidia ukuaji wa uchumi katika kanda ya Magharibi. Hilo ni tawi la 25 kwa mkoani Geita na la 229 nchini Tanzania.
Akizungumza wakati wa hafla ya kuzindua tawi hilo, mgeni rasmi Mkuu wa mkoa wa Geita Eng. Gabriel Luhumba amesema ufunguzi wa tawi hilo umekuja wakati muafaka kwa kuwa ofisi za serikali zinampango wa uchumi wakimkakati ambao utafanya Geita kuwa chachu ya maendeleo nchini.
Akiongea na wananchi wa wilaya ya Mbogwe Eng. Gabriel Luhumba pia ametoa rai kwa wananchi kubadilika na kuacha mazoea ya kuweka pesa majumbani na kuwataka kuwa na tabia ya kuweka benki na kwenye taasisi za fedha.
Eng.Luhumba alisema wananchi wa mkoa wa Geita wenye neema nyingi ya madini aina ya dhahabu wamekuwa na tabia ya kutunza fedha zao nyumbani hali ambayo imekuwa ni hatari kwa usalama wa maisha yao na kuwataka kuacha tabia hiyo.
Alisema mazoea na tabia ya kuweka fedha kwenye vitanda , kuchimbia chini au kwenye mazizi ya mifungo ilishapitwa na wakati kwa kipindi hiki na kuwataka vipato vyao vya pesa wanapopata kwenda kuziweka benki na kwenye taasisi za zinazotunza fedha.
“Ndugu zangu wananchi uhai katika maisha yetu ni bora sana, katika familia zetu , tabia ya kuendelea kukaa na fedha majumbani kwetu ni hatari sana kwa sababu unaweza kuvamiwa na watu waharifu wakawashambulia na kupoteza maisha kwa hiyo rai yangu mnapopata pesa iwe hata kidogo lazima tupeleka kuziweka benki,, Alisema Eng.Luhumba.
Eng. Luhumba katika hotuba yake alitoa wito kwa wananchi wa wilaya ya Mbogwe kutumia fursa zinazotolewa na benki hiyo kujiletea mafanikio kiuchimi katika maisha yao na kuwataka kuwa wakopaji wazuri wa mikopo na kulejesha kwa wakati.
Mbali na kuipongeza menejimenti ya benki hiyo, aliipa changamoto ya kuhakikisha inaweza kuandaa Kongamano la biashara katika mkoa wa Geita ilikuwapa msasa wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla kuhusu kuchangamkia fursa zilipo mkoani humo ilikuhakikisha wananchi wanapata maendeleo yenye tija ndani na nje ya kanda ya Magharibi na Afrika Mashariki.
Mkuu wa wilaya ya Mbogwe Martha Mkupasi alisema anaishukuru benki ya NMB kwa kuwasogezea huduma za kibenki kutokana na kuwa wananchi walikuwa na kilio cha siku nyingi kwa serikali kuitaka benki kwa sababu walikuwa wasafiri zaidi ya kilimita 50 kufaata huduma hizo wilaya jirani za Bukombe na Kahama mkoa wa Shinyanga.
Mkupasi alisema kufunguliwa kwa tawi hilo la benki hiyo kumewaondolea aza waliyokuwa wanaipata kusafiri na fedha umabari mrefu hali iliyokuwa inahatarisha maisha yao kwa kuhofia kuvamiwa na majambazi , kwa kusogezewa huduma hiyo na kuwahimiza kutumia fursa hiyo kuichumi na kujiletea maendeleo.
Awali katika hotuba yake mkuu wa kitengo cha biashara wa benki ya NMB , Donatus Richard alisema sasa tawi hilo ni la 229 kwa nchi zima na huo ni wajibu wao katika kuwasogezea huduma hizo wananchi, wafanyabiashara wa dogo, wa kati na wakubwa ili kuwawezesha watu kupata mitaji kwa ajili ya biashara na shughuli mbalimbali nalengo la kuwanyanyua kiuchumi na kuwaomba wachangamikie fursa zionazotolewa na benki ili kujiletea maendeleo.
No comments:
Post a Comment