Maalim akiwa na Kiongozi wa ACT Wazalendo, Zito Kabwe. |
Kwa uamuzi huo Mahakama imekubaliana na uamuzi wa Msajili wa Vyama vya Siasa nchini wa kumtambua kwa barua Prof. Lipumba kuwa bado ni Mwenyekiti halali wa Chama cha CUF.
"Shusha tanga, pandisha tanga safari iendelee,' alisema Maalim Seif wakati akitangaza uamuzi wake wa kuhamia ACT Wazalendo leo. MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam imekubaliana na uamuzi wa Msajili wa Vyama vya Siasa wa kumtambua Profesa Ibrahimu Lipumba kuwa ndiye bado Mwenyekiti halali wa Chama cha Wananchi (CUF) na kumaliza mvutano uliyekuwepo kati yake na Katibu mkuu wa CUF, Maalim Seif Hamad.
Kwa maamuzi hayo, Mahakama hiyo imetupilia mbali maombi yaliyofunguliwa na Katibu wa CUF, Maalim Seif akiiomba mahakama kutoa amri ya kubatilisha barua ya Msajili wa vyama ya kumtambua Profesa Lipumba kuwa Mwenyekiti.
Akitoa uamuzi huo, Jaji Benhaji Juma Masoud alisema, mjibu maombi namba moja, Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, alikuwa na mamlaka ya kutoa ushauri na maamuzi kwa chama husika ili wahusika wachukue hatua zinazopaswa.
Katika shauri hilo, Maalim Seif aliwakilishwa na Wakili Juma Nassoro na Loveness Denis huku wajibu maombi ni Msajili wa Vyama vya Siasa, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Profesa Lipumba na wanachama wengine wa CUF waliwakilishwa na Mashaka Ngole.
Jaji Msaoud alisema, baada ya migogoro iliyotokea ndani ya chama hicho, Msajili aliandika barua kutoa msimamo na ushauri kwa Uongozi wa juu wa CUF ambapo katika barua hiyo ilimtambua Profesa Lipumba kuwa mwenyekiti wa chama hicho.
Amesema, majukumu ya Msajili hayaishii katika kusajili vyama pekee bali pia anayo mamlaka ya kufuta vyama na kutoa msimamo kitu ambacho ndio alichokifanya. Hivyo kanuni ambazo waleta maombi wanataka zirejewe na kuelekeza kile wanachokiona zinatupiliwa mbali na kuongeza kuwa hatatoa amri yoyote kuhusu gharama.
No comments:
Post a Comment