TEKNOLOJIA YA MAWASILIANO INAVYOCHOCHEA MALENGO YA MAENDELEO NCHINI - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Monday, 18 March 2019

TEKNOLOJIA YA MAWASILIANO INAVYOCHOCHEA MALENGO YA MAENDELEO NCHINI


Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi Atamizi ya Kuleta Ubunifu Kupitia Teknolojia (DTBI), Dk. George Mulamula, akizungumza katika uzinduzi wa ripoti iliyoangalia mabadiliko ya kidigitali nchini Tanzania na mchango wa teknolijia za simu za mikononi kuchochea maendeleo.

Mwakilishi wa makampuni ya simu akizungumza katika uzinduzi huo, Bi. Beatrice Sengano.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Kuendeleza Sekta ya Fedha Tanzania, Bw. Sosthenes Kewe akizungumza katika haafla hiyo iliyofanyika Ukumbi wa Mwalimu Julias Nyerere jijini Dar es Salaam leo.

Mr. Kenechi Okeleke mchambuzi kutoka GSMA akielezea utafiti wa ripoti hiyo.

Na Mwandishi Wetu,

IMEELEZWA kuwa teknolojia ya mawasiliano nchini Tanzania imechangia kwa kiasi kikubwa kuchochea maendeleo katika nyanja mbalimbali. Hayo yamebainishwa katika uzinduzi wa ripoti iliyoangalia mabadiliko ya kidigitali nchini Tanzania na mchango wa teknolijia za simu kuchochea maendeleo.

Akizungumza leo jijini Dra es Salaam mara baada ya uzinduzi wa ripoti hiyo ya utafiti, Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi Atamizi ya Kuleta Ubunifu Kupitia Teknolojia (DTBI), Dk. George Mulamula, wao kama wadau wameangalia ni jinsi gani ubunifu na ujasiliamali unaweza kusaidia katika sekta ya mawasiliano.

Alisema teknolojia ya mawaasiliano hainabudi kuangalia namna gani itaendelea kuleta mabadiliko kwa mwananchi wa kawaida hasa wajasiliamali ili kuchochea vipato vyao na taifa kwa ujumla.

"Ipo haja ya kuangalia mwananchi wa kawaida anawezaje kuitumia teknolojia ya mawasiliano kuchochea kipato chake, ama kuleta mabadiliko kiuchumi...hasa ukizingatia ripoti inabainisha teknolojia ya mawasiliano kutoa mchango katika pato la taifa kwa asilimia 11.

Pamoja na hayo utafiti umeonesha kukua kwa kasi kwa idadi ya watumiaji wa simu za mkononi na intaneti kwa ujumla hali inayoongeza matumaini kukua kwa kasi kwa sekta husika. Hadi sasa idadi ya watumiaji wa simu za mkononi nchini inakadiriwa kufikia watu milioni 25.2 ukilinganisha na ile ya watu milioni 5 kwa waka 2007.

Ripoti imebainisha makampuni ya simu za mkononi kwa ujumla kupitia huduma zake anuai yamekuwa yakisaidia kuchochea maendeleo ya kiuchumi kwa jamii, hasa katika sekta za elimu, afya, huduma za fedha na mawasiliano kwa ujumla.

Akizungumza mwakilishi wa makampuni ya simu katika uzinduzi huo, Beatrice Sengano alisema wanapata faraja hasa baada ya kuona utafiti unatambua mchango wa makampuni hayo katika kuisaidia jamii kwenye nyanja tofauti na wataendelea kuwa wabunifu zaidi kutoa huduma kwa manufaa ya jamii.

Sehemu ya wadau wakiwa katika uzinduzi wa hafla hiyo.

No comments:

Post a Comment