`
Ofisa Ardhi wa Shirika la The Winamwanga Cultural Heritage Association (TWCHA) , Ivy Mwansepe, akimkabidhi taarifa ya kazi ya shirika hilo ya mwezi Novemba na Desemba mwaka 2017, Mgeni rasmi, Ofisa Kilimo wa Kata ya Kurui, Baraka Budangi, wakati wa mkutano wa Madiwani na wadau wa kilimo uliofanyika juzi wilayani Kisarawe mkoani Pwani juzi. Kulia ni Mratibu wa kilimo wa shirika hilo, Saidi Simkonda.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Zegero, Abdallah Binda akifungua mkutano huo.
Katibu wa shirika hilo, Richard Ng'wandu, akizungumza kwenye mkutano huo. Kulia ni Mwenyekiti wa shirika hilo, Isabela Luoga na Ofisa Ardhi Ivy Mwansepe.
Mkazi wa Kijiji cha Zegero Marcelina Mziray, akichangia jambo kwenye mkutano huo. Kutoka kulia ni Zulfa Tarazo na Mwenyekiti wa Kikundi cha Wakulima wa Kijiji cha Zegero, Fatuma Ali.
Mwenyekiti wa Kikundi cha Wakulima wa Kijiji cha Zegero, Fatuma Ali, akizungumza.
Mratibu wa Mradi wa Kilimo kutoka Taasisi hiyo, Saidi Simkonda, akizungumza.
Mwenyekiti wa shirika hilo, Isabela Luoga, akizungumza.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Kilimo Joint, Linda Byaba, akichangia jambo kwenye mkutano huo. Kushoto ni mdau wa kilimo, Salama Somboka
Na Dotto Mwaibale, Kisarawe
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Suleiman Jafo anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye hafla ya uzinduzi wa Jukwaa la Kilimo utakaofanyika Kata ya Kurui wilayani Kisarawe mkoani Pwani.
Katika uzinduzi huo Waziri Jafo ambaye ni kiongozi wa juu wa serikali katika wilaya hiyo atakabidhi hati miliki za kimila za ardhi 315 ambazo zimeandaliwa na Shirika la The Winamwanga Cultural Heritage Association (TWCHA) katika maeneo ya vijiji vya Mafizi, Gwata, Kidugalo, Mtakayo, Zegero na Marui.
Akizungumza katika mkutano wa madiwani na wadau wa maendeleo ya kilimo wakati akitoa taarifa ya kazi zilizofanywa na shirika hilo kwa mwezi Novemba na Desemba 2017 Mratibu wa Mradi wa Kilimo kutoka Taasisi hiyo, Saidi Simkonda alisema waliona ni busara Waziri Jafo awe mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo kwa kuzingatia kuwa yeye ni mwenyeji wa eneo hilo.
"Tayari mchakato wa kumuomba Waziri Jafo kuwa mgeni rasmi tumeufanya tunachosubiri ni majibu yake kwani tunapenda kufanya tukio hilo mwanzoni mwa mwezi wa kwanza mwaka 2019" alisema Simkonda.
Alisema mpaka sasa wana wanachama 750 kati ya hao 250 ni walemavu ambao wanamashamba katika kata hizo ambayo yanafanyiwa mchakato wa kupata hati miliki za kimila za ardhi huku 315 zikiwa tayari.
Alisema katika kipindi hicho shirika hilo o kwa kushirikiana na Halmshauri ya `Wilaya ya Kisarawe limeweza kutoa ushauri mbalimbali kwa watu Wanaotaka `Kuendeleza maeneo yao, kufanya mikutano na wananchi juu ya kuwaelimisha namna ya kuipandisha ardhi thamani kwa kupima mashamba yao na `kupata hati ya hakimiliki ya kimila.
Alitaja baadhi ya changamoto kuwa ni wananchi wengi wa wilaya hiyo kutokuwa na elimu ya umiliki wa mashamba na umuhimu wa kumiliki haki ya hati miliki ya kimila na watendaji wa vijiji kutojua makusanyo ya fedha za kodi ya ardhi ya kijiji kuwa zinawakilishwa wapi.
Alisema katika makusanyo ya kodi za ardhi shirika lilishauri ni vyema kama Serikali za vijiji havina vitabu vya risiti ni vizuri wananchi wapewe akaunti za Serikali za vijiji kufanya malipo ya tozo za ardhi au makusanyo yoyote kwa maendeleo ya kijiji husika.
Katika mkutano huo madiwani hao waliwakilishwa na Ofisa Kilimo wa Kata ya Kurui Baraka Mudangi.
No comments:
Post a Comment