NDEGE MPYA YA AIRBUS 220 - 300 ILIYONUNULIWA NA SERIKALI YA TANZANIA. - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Monday, 24 December 2018

NDEGE MPYA YA AIRBUS 220 - 300 ILIYONUNULIWA NA SERIKALI YA TANZANIA.

Ndege mpya aina ya Airbus 220-300 ambayo imenunuliwa na Serikali ikimwagiwa maji ikiwa ni ishara ya karibu na heshima (Water salute) kwa mara ya kwanza katika ardhi ya Tanzania Uwanja ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Desemba 23,2018.
Katibu mkuu kiongozi Balozi Dk. John Kijazi pamoja na katibu mkuu wa Wizara ya Ujenzi mawasiliano na Uchukuzi Dk. Leonard Chamuriho wakisaini mkataba wa makabidhiano ya Ndege mpya ya Airbus 220-300 itakayokabidhiwa katika shirika la ndege la Tanzania mbele ya   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pamoja na viongozi wengine wakishuhudia kabla ya kuwasili kwa Ndege mpya aina ya Airbus 220 - 300 ambayo imenunuliwa na Serikali.Hafla iliyofanyika katika Uwanja ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Desemba 23,2018.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akihotubia kabla ya kuwasili kwa Ndege mpya aina ya Airbus 220 - 300 ambayo imenunuliwa na Serikali.Hafla iliyofanyika katika Uwanja ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Desemba 23,2018.
Viongozi na Wafanyakazi wa Shirika la ndege la Tanzania (ATCL) wakiwapongeza na kuwakaribisha wenazao amabao walitoka safarai na Ndege mpya aina ya Airbus 220 - 300 ambayo imenunuliwa na Serikali mara ya kuwasili katika ardhi ya Tanzania Uwanja ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Desemba 23,2018.

No comments:

Post a Comment