NMB YATOA MSAADA WA VITANDA NA MASHUKA HOSPITALI YA MNAZI MMOJA, ZANZIBAR - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Thursday, 6 December 2018

NMB YATOA MSAADA WA VITANDA NA MASHUKA HOSPITALI YA MNAZI MMOJA, ZANZIBAR

Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Ayoub Mohamed Mahmoud (alievaa tai rangi ya bluu) akimkabidhi  Kitanda na Mashuka Mkurugenzi Mtendaji Hospitali ya Mnazimmoja Dkt. Ali Salum (kulia) Mbunge wa viti Maalum Wanawake CCM Asha Abdalla Juma, Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Zanzibar Abdalla Duchi na (kushoto) Meneja Uhusiano Faraja Kaziulaya kutoka Dar es Salam.

BENKI ya NMB imetoa msaada wa vitanda maalum vya kujifungulia pamoja na mashuka katika Hospitali ya Mnazi mmoja, mjini Zanzibar vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 10. Vifaa hivyo vimepokelewa na Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi, Ayoub Mohamed Mahmoud ambaye alikuwa ni mgeni rasmi katika hafla hiyo. 

Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Zanzibar Abdalla Duchi akimkabidhi Mashuka na Kitanda Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Ayoub Mohamed Mahmoud (kulia) ni Mbunge wa viti Maalum Wanawake CCM Asha Abdalla Juma (Mshua) na Mkurugenzi Mtendaji Hospitali ya Mnazimmoja Dkt. Ali Salum.

Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Zanzibar Abdalla Duchi akizungumza na Mgeni Mwalikwa pamoja na Watendaji wa Hospitali ya Mnazi Mmoja kabla ya kukabidhi msaada wa Vitanda nane (8) na mashuka mia moja na ishirini (120) kwaajili ya Hospitali hiyo.

Mbunge wa viti Maalum Wanawake CCM Asha Abdalla Juma (Mshua) na Mdau wa mambo ya afya akizungumza katika hafla ya kukabidhi msaada wa Vitanda na Mashuka kwaajili ya huduma za Kujifungulia katika Hospitali Kuu ya Mnazimmoja jengo la Dodoma.


No comments:

Post a Comment