HALOTEL KUWAZAWADIA WATEJA NA CHRISMAS BANG BANG - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Thursday, 6 December 2018

HALOTEL KUWAZAWADIA WATEJA NA CHRISMAS BANG BANG

 Mkuu wa Mawasiliano wa Kampuni ya Simu ya Halotel, Mhina Semwenda, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu kampuni hiyo kuelekea msimu huu wa sikukuu kutoa punguzo la zaidi ya asilimia sitini (60%) katika kifurushi chake cha siku ambapo sasa wateja watapata GB 2 kwa shilingi 2000 ikiwa ni gharama nafuu zaidi ya vifurushi vya intaneti na kutoa punguzo kubwa la smartphone aina ya OXE 101. Kulia ni Meneja Uhusiano wa Halotel, Stella Pius na Meneja Mawasiliano, Hindu Kanyamala.

Mkuu wa mawasiliano wa Halotel, Mhina Semwenda akizungumza na waandishi wa Habari katika Makao Makuu ya kampuni hiyo kuhusu Ofa mpya ya Krismasi na mwaka Mpya iliyozinduliwa leo inayokwenda kwa jina la “Christmas Bang Bang” namna itakayowawezesha wateja wote wa Halotel kupata GB2 za intaneti kwa sh. 2000 tu.na pia wateja wote watapata zawadi wataaakapofika maduka yetu yote nchi nzima. Pamoja nae katika picha, (kulia) na Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo Stella Pius.

 Wapiga picha wakichukua tukio hilo.


Mkutano na wanahabari ukiendelea.

Na Mwandishi Wetu

 KATIKA kuelekea msimu huu wa sikukuu kampuni ya simu ya Halotel imetoa punguzo la zaidi ya asilimia sitini (60%) katika kifurushi chake cha siku ambapo sasa wateja watapata GB 2 kwa shilingi 2000 ikiwa ni gharama nafuu zaidi ya vifurushi vya intaneti na kutoa punguzo kubwa la smartphone aina ya OXE 101.


Akizungumzia punguzo hilo kubwa, Mkuu wa Mawasiliano wa Halotel, Mhina Semwenda amesema ofa hiyo imezingatia mahitaji makubwa ya wateja wa mtandao huo katika msimu huu wa sikukuu na kutoa nafasi kwa wateja kupeana taarifa na fursa ya kutembelea mitandao mbali mbali ya kijamii.


“Msimu wa sikuu kuu unatoa fursa kwa wateja wetu, kutembelea maeneo mbalimbali ya nchi, wengi wanahitaji taarifa za maeneo wanayoenda, au wanaweza kupenda kushare matukio au hata kupata muda mwingi wa kutumia simu zao, hivyo tumeonelea ni vyema sasa, tuwape sababu ya kufurahia msimu huu wa sikukuu kwa kuwapatia ongezeko kubwa kabisa la GB za intaneti, Alisema Mhina na kuongeza.


Jambo kubwa kabisa la kuwahakikishia wateja wetu ni kuwa maeneo yote watakayo kwenda iwe vijijini au sehemu nyinginezo, watakuwa pamoja nasi na watakuwa na uhakika wa kutumia huduma zetu kutoka katika mtandao wetu uliosambaa Zaidi hapa nchini kwa kufikia Zaidi ya asilimia 95% ya Watanzania.

“Huduma hii ni zawadi kwa wateja wote wa Halotel nchini msimu huu wa sikukuu kwa kuendelea kutumia intanet yenye kasi zaidi nchini kipindi hiki cha mapumziko wakati wowote, ambapo kwa kujiunga na huduma ya CHRISTMAS BANG BANG mteja atapata  kifurushi cha intenet cha GB 2 cha siku kwa sh 2000 tu tofauti na kirushi cha kawaida ambacho mteja angepata GB 1.3 kwa siku kwa sh 2000.
Zaidi tunapenda kuwakumbusha watanzania na wateja wetu wote wataweza kujipatia zawadi mbali mbali  pindi watakapo fika kwenye maduka yetu ya Halotel nchi nzima katika  kipindi msimu huu wa sikukuu. Tunatakia watanzania na wateja wa Halotel waipokee zawadi ya CHRISTMAS BANG BANG kutoka Halotel,. alisema Kanyamala na kuongeza.

Tunawahakikishia wateja wetu kuwa tutafanya msimu huu wa sikukuu kuwa Bang Bang kwa kuendelea kuboresha huduma zetu.

No comments:

Post a Comment