Waziri wa nchi ofisi ya Rais anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Watu wenye ulemavu Mhe. Jenesta Mhagama (Mb.) akimkabidhi Tuzo Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi (TUGHE- MSD), John Gabriel katika hafla iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa MSD wakionesha tuzo hizo katika hafla hiyo.
Kaimu Mkurugenzi wa Fedha na Mipango wa MSD, Bw.Soko Mwakalobo na Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala Bi.Victoria Elangwa wakionesha tuzo hizo.
Na Dotto Mwaibale
BOHARI ya Dawa (MSD) imeshinda tuzo tatu za Mwajiri bora za ATE mwaka huu (2018) na kwa mara ya kwanza kuingia kwenye kinyang'anyiro cha kumi bora kwa mwajiri bora Tanzania.
MSD ni kati ya waajiri 59 waliofikia hatua ya mchujo huo na tuzo walizoshinda MSD ni pamoja na Mwajiri Bora anayeangalia USTAWI wa wafanyakazi (employee WELLNESS), Mwajiri Bora wa kizalendo (Overall best local winner) na Mwajiri Bora katika utumishi wa Umma.
Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa Bohari ya Dawa (MSD) Bi.Victoria Elangwa amesema ushindi huo unatokana na ushirikiano madhubuti kati ya wafanyakazi menejimenti na Wizara, utekelezaji mzuri wa mpango mkakati wa MSD pamoja na mahusiano bora na chama cha wafanyakazi.
Mkurugenzi Mkuu wa MSD Bw. Laurean Rugambwa Bwanakunu amefurahishwa na tuzo hizo na kuwapa rai wafanyakazi wote kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili wapate tija zaidi kama kauli mbiu ya taasisi inavyosema; *"Tumedhamiria kuokoa maisha yako"*.
Tuzo hizo zilitolewa jijini DSM na Waziri wa nchi ofisi ya Rais anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Watu wenye ulemavu Mhe. Jenesta Mhagama (Mb.)
No comments:
Post a Comment