WAZIRI WA KILIMO HASUNGA AAGIZA WALIOKOPA KWENYE SACCOS KULIPA MADENI ...! - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Saturday, 15 December 2018

WAZIRI WA KILIMO HASUNGA AAGIZA WALIOKOPA KWENYE SACCOS KULIPA MADENI ...!


Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akisisitiza jambo wakati wa kikao cha kazi alipokuwa akizungumza na viongozi wakuu wa vyama vya Akiba na Mikopo (SACCOS) sambamba na Vyama vya Msingi vya Ushirika vilivyopo katika Mkoa wa Mtwara katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, tarehe 14 Disemba 2018.

Viongozi wakuu wa vyama vya Akiba na Mikopo (SACCOS) sambamba na Vyama vya Msingi vya Ushirika vilivyopo katika Mkoa wa Mtwara wakifatilia hotuba ya Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akisisitiza jambo wakati wa kikao cha kazi katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, tarehe 14 Disemba 2018.

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akisisitiza jambo wakati wa kikao cha kazi alipokuwa akizungumza na viongozi wakuu wa vyama vya Akiba na Mikopo (SACCOS) sambamba na Vyama vya Msingi vya Ushirika vilivyopo katika Mkoa wa Mtwara katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, tarehe 14 Disemba 2018.

Na Mathias Canal, Mtwara

WAZIRI wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameagiza kurejeshwa ndani ya miezi mitatu madeni yote yaliyokopwa kwenye vyama vya akiba na mikopo (SACCOS).

Alisema kuwa mwananchi watakaoshindwa kutii maelekezo hayo katika kukamilisha deni lake ndani ya miezi mitatu hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

“Nataka kila aliyekopa kwenye Saccos arejeshe deni lake kwa kufuata utaratibu wa makubaliano na kama wasipotekeleza ndani ya miezi mitatu niliyotoa serikali itaagiza wahusika wote kukamatwa maana dawa ya deni ni kulipa” Alisisitiza

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga ametoa agizo hilo tarehe 14 Disemba 2018 wakati wa kikao cha kazi katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara alipokuwa akizungumza na viongozi wakuu wa vyama vya Akiba na Mikopo (SACCOS) sambamba na Vyama vya Msingi vya Ushirika vilivyopo katika Mkoa wa Mtwara.

Kikao hicho kimehudhuriwa pia na Kaimu Mrajisi wa vyama vya Ushirika nchini, Mkaguzi wa vyama vya ushirika na Saccos, Kaimu Mrajisi msaidizi wa mkoa wa Mtwara, Wenyeviti na watendaji wa SACCOS pamoja na vyama vya msingi vya ushirika vilivyopo mkoani Mtwara.

Mhe Hasunga amelitaka Shirika la Ukaguzi wa Hesabu za Vyama vya Ushirika (COASCO) kutimiza majukumu yake kwa weledi kwa kukagua na kuhakikisha vyama vyote vinafunga mahesabu huku akitaka vyama ambavyo sio hai kuchukuliwa hatua.
Pia ameagiza kila chama Tanzania kiwe na daftari la wanachama walio hai na wafu sambamba na kuhakikisha kuwa viongozi wote wawe na maadili na uwezo wa kuvisimamia vyama vyao ipasavyo.

Katika hatua nyingine alimtaka Mrajis wa ushirika Tanzania Bw Tito Haule kuwasilisha mpango kazi wa namna ya kukutana na wanachama wa ushirika nchi nzima katika kutatua changamoto zao. “ Na ni lazima taarifa itengenezwe ikionyesha idadi ya vyama mlivyokutana navyo na kueleza ni mambo gani mmezungumza kila mwezi” Alisema

Aliongeza kuwa Viongozi ni lazima kutoa mapendekezo ya mabadiliko ya sheria ya Ushirika itakayosaidia kuondoa usumbufu kwenye ushirika ili uendelee kuwa mkombozi wa wananchi. “Mje na mfumo wa namna ya kuwasaidia wananchi kupata pembejeo bila kuingia madeni yasiyokuwa na tija” Alisisitiza

No comments:

Post a Comment