Mmoja wa wakilishi wa Kundi la
Wasapu la Wanafunzi wahitimu kidato cha nne mwaka 2000 katika Sekondari ya
Majengo iliyopo mkoani Kilimanjaro, Eng. Willbard Gandu (kulia) akikabidhi sehemu ya
msaada wa wanafunzi hao katika kituo yatima cha ‘Green Pastures’ cha jijini Dar
es Salaam.
Mmoja wa wakilishi wa Kundi la
Wasapu la Wanafunzi wahitimu kidato cha nne mwaka 2000 katika Sekondari ya
Majengo iliyopo mkoani Kilimanjaro, Injinia Eng. Maeda (kulia) akimkabidhi mmoja wa watoto wa kituo yatima cha ‘Green Pastures’ cha jijini Dar
es Salaam sehemu ya msaada uliotolewa na wanafunzi hao.
Mmoja wa wakilishi wa Kundi la Wasapu la Wanafunzi wahitimu kidato cha nne mwaka 2000 katika Sekondari ya Majengo iliyopo mkoani Kilimanjaro, Bw. Oswald (kulia) akimkabidhi mmoja wa watoto wa kituo yatima cha ‘Green Pastures’ cha jijini Dar es Salaam sehemu ya msaada uliotolewa na wanafunzi hao. |
Sehemu ya msaada uliokabidhiwa na wawakilishi wa kundi mkoani Kilimanjaro Kituo cha 'Hope Village For Orphans and Vulnerable Children' cha mkoani Kilimanjaro. |
KUNDI la Wasapu la Wanafunzi
wahitimu kidato cha nne mwaka 2000 katika Sekondari ya Majengo iliyopo mkoani
Kilimanjaro limetembelea vituo vitatu vya watoto wanaoishi katika maazingira
maagumu na kutoa misaada mbalimbali ikiwa ni kuwafariji watoto hao.
Vituo vilivyonufaika na misaada hiyo
ni pamoja na Kituo cha watoto yatima ‘Green Pastures’ cha jijini Dar es Salaam,
Kituo cha watoto yatima cha ‘Tanzania Childrens Rescue Centre (TCRC)’ jijini
Mwanza na Kituo cha 'Hope Village For Orphans and Vulnerable Children' cha mkoani Kilimanjaro.
Akizungumzia msaada huo mmoja wa
viongozi wa kundi hilo la wanafunzi waliohitimu Sekondari ya Majengo, Joachim
Mushi alisema wanafunzi hao walichanga fedha kwa ajili ya kuwatembelea wahitaji
ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 4 tangu kuanzishwa kwa kundi hilo.
“…Wanakikundi waliamua kuchangishana
fedha kwa ajili ya kuwatembelea wahitaji na kutoa chochote kwa lengo la
kuwafariji yatima, na misaada kugawanywa katika mikoa mitatu yenye wawakilishi yaani
Mwanza, Dar es Salaam na Mkoa wa Kilimanjaro…hii ni sehemu ya maadhimisho ya
miaka minne ya kundi ambalo tulilianzisha 2014,” alisema Bw. Mushi.
Msaada uliyotolewa ni mifuko ya unga
wa sembe, mchele, sukari, maharage, sabuni za kufulia na kuogea, mafuta ya
kupikia, madaftari, vyombo vya kutumia pamoja na peni.
Vingine ni pamoja na Dawa za meno, miswaki,
biskuti, juisi, maji ya kunywa, mikate, majani ya chai, viatu pamoja na nguo mbalimbali za watoto vyote
vikiwa na zaidi ya thamani ya zaidi ya milioni 1.8.
Eng. Willbard Gandu (aliyesimama) akizungumza na watoto wa kituo yatima cha ‘Green Pastures’ cha jijini Dar es Salaam kuwafariji. |
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha watoto yatima ‘Green Pastures’, Mchungaji Douglas Kiseu (wa kwanza kulia) akiwatembeza wawakilishi katika kituo chake mara baada ya kukabidhi msaada wa kundi lao. |
Picha ya pamoja ya wawakilishi wa Dar es Salaam wa kundi la Wasapu la Wanafunzi wahitimu kidato cha nne mwaka 2000 Sekondari ya Majengo iliyopo mkoani Kilimanjaro |
No comments:
Post a Comment