KAIMU Balozi wa Marekani nchini Tanzania Dkt. Inmi
Patterson na Waziri wa Nchi Ofisi ya
Makamu wa Rais wa Muungano na Mazingira Ndugu January Makamba wamezindua mradi
utakaogharimu kiasi cha dola za kimarekani milioni 20 ili kuboresha usimamizi
katika kuhifadhi mazingira kwenye ukanda wa magharibi mwa Tanzania. Mradi
huu wa uhifadhi wa mazingira
unafadhiliwa na Serikali ya Marekani kupitia Shirika lake la Maendeleo ya
Kimataifa (USAID) na utatekelezwa kwa ushirikiano wa pamoja na Taasisi ya Jane
Goodall (JGI).
Mradi huu mpya utasaidia watu wa Mikoa ya Kigoma
na Katavi, pamoja na serikali za mitaa, katika utekelezaji wa mipango ya
matumizi bora ya ardhi na utakaonufaisha vijiji 104.
Mradi huu wa Uhifadhi wa Mazingira umeundwa
kulinda mazingira wakati pia unasaidia wananchi katika shuhuli za kujikimu
kiuchumi na maisha bora kama vile uzalishaji wa kahawa na utalii asili kwa
ajili ya watanzania. Taasisi ya Jane Goodall itafanya kazi kwa karibu na jamii
ili kuhamasisha mazoea endelevu zaidi ya usimamizi wa ardhi na kukuza elimu ya
mazingira, kwa kutumia majukwaa kama vile mradi
iliyofanikiwa sana ya Roots na Shoots ya Taasisi ya Jane Goodall.
Zaidi ya hayo, kama sehemu ya ruzuku hii, Taasisi
ya Jane Goodall itaendelea kufanya kazi kwa kushirikiana na Serikali ya
Tanzania katika kuunda mifumo imara zaidi katika kuhifadhi na kulinda sokwe
walioko ndani na nje ya maeneo tengefu.
No comments:
Post a Comment