RAIS DK MAGUFULI ASHIRIKI MISA MAADHIMISHO JUBILEI YA MIAKA 150 YA UINJILISHAJI, AFYA NA ELIMU, BAGAMOYO - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Sunday 4 November 2018

RAIS DK MAGUFULI ASHIRIKI MISA MAADHIMISHO JUBILEI YA MIAKA 150 YA UINJILISHAJI, AFYA NA ELIMU, BAGAMOYO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Muadhama Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Nairobi John Kardinal Njue ambaye aliongoza Misa Takatifu ya Jubilei ya  Miaka 150 ya Uinjilishaji, Afya na Elimu Bagamoyo mkoani Pwani.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Waumini mbalimbali wa Kanisa Katoliki, Maaskofu pamoja na Wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi  katika Maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 150 ya Uinjilishaji, Afya na Elimu mara baada ya Misa iliyofanyika Bagamoyo Mkoani Pwani.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Maaskofu wa Kanisa Katoliki mara baada ya Misa ya ya Maadhimisho ya Miaka 150 ya Uinjilishaji, Afya na Elimu Bagamoyo mkoani Pwani.

Baadhi ya Maaskofu mbalimbali wa Kanisa Katoliki wakiwa katika Misa Takatifu ya Jubilei ya  Miaka 150 ya Uinjilishaji, Afya na Elimu Bagamoyo mkoani Pwani.

Baadhi ya Maaskofu mbalimbali wa Kanisa Katoliki wakiwa katika Misa Takatifu ya Jubilei ya  Miaka 150 ya Uinjilishaji, Afya na Elimu Bagamoyo mkoani Pwani.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akizungumza jambo na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Benjamini Mkapa kabla ya kuanza kwa Misa takatifu ya Jubilei ya  Miaka 150 ya Uinjilishaji, Afya na Elimu Bagamoyo mkoani Pwani. PICHA NA IKULU

Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Benjamini Mkapa pamoja na Spika Mstaafu Anne Makinda wakiwa katika Misa takatifu ya ya Jubilei ya  Miaka 150 ya Uinjilishaji, Afya na Elimu Bagamoyo mkoani Pwani.

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. John Pombe Magufuli Novemba 4, 2018 ameungana na Waumini wa Kanisa Katoliki hapa nchini kuadhimisha Jubilei ya miaka 150 ya Uinjilishaji Tanzania Bara.
Misa Takatifu ya maadhimisho ya Jubilei hiyo ambayo imefanyika Bagamoyo Mkoani Pwani ambako Ukristo uliingia mwaka 1868  imeongozwa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Nairobi nchini Kenya Mwadhama John Kardinali Njue.
Misa hiyo imehudhuriwa na Mke wa Rais Mhe. Mama Janeth Magufuli, Rais Mstaafu Mhe. Benjamin William Mkapa, Spika Mstaafu Mhe. Anne Makinda, Maaskofu wa Majimbo yote ya Kanisa Katoliki hapa nchini na nchi jirani, Mapadre, Watawa na waumini wa Kanisa hilo kutoka majimbo yote hapa nchini.
Akizungumza katika Misa hiyo, Mhe. Rais Magufuli amelipongeza Kanisa Katoliki kwa mchango lililoutoa kuwahudumia Watanzania kiroho na kutoa huduma za kijamii tangu miaka 150 iliyopita na ameahidi kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na Kanisa katika kudumisha amani na upendo na kuwaletea wananchi maendeleo.
Mhe. Rais Magufuli amewashukuru Maaskofu, Mapadre, Watawa na viongozi wote wa Kanisa Katoliki kwa namna wanavyoshirikiana na Serikali na Madhehebu mengine ya dini katika kuleta maendeleo na kuimarisha ustawi wa jamii bila kubagua na amewaomba waendelee kukemea vitendo viovu vikiwemo uvunjifu wa amani, rushwa, ufisadi na ubakaji.
Aidha, Mhe. Rais Magufuli amewashukuru wananchi wa Bagamoyo kwa kuupokea Ukristo ambao uwepo wake umeleta manufaa makubwa kwa Watanzania na ameahidi kuwa Serikali itashirikiana na viongozi wa Kanisa hilo kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili.
Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) Mhashamu Gervas Nyaisonga amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kuungana na Kanisa Katoliki katika Jubilei hiyo, amempongeza kwa kazi nzuri ya kutimiza ahadi alizozitoa kwa Watanzania katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wake na ameahidi kuwa Kanisa Katoliki litaendelea kuliombea Taifa na kushirikiana na Serikali.

No comments:

Post a Comment