VIKUNDI VILIVYOPEWA MIKOPO VYAPATA TENDA HALMASHAURI - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Wednesday, 14 November 2018

VIKUNDI VILIVYOPEWA MIKOPO VYAPATA TENDA HALMASHAURI

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (kulia) akitoa hundi ya shilingi Milioni 3.5 kwa kikundi cha Perfect Group kinachotengeneza chaki Mnaipaa ya Sumbawanga. 

Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dkt. Khalfan Haule (kushoto) akipita na mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo katika vikundi mablimbali vilivyoleta bidhaa katika hafla hiyo ya vikundi vilivyopewa mkopo na Manispaa ya Sumbawanga.

MKURUGENZI wa Manispaa ya Sumbawanga Jacob Mtalitinya amevihakikishia ajira na masoko vikundi 21 vya vijana wanawake na walemavu kutoka katika ofisi ya halmashauri hiyo ili kuongeza chachu ya maendeleo ya viwanda na kuongeza ajira na hatimae kuinua vipato vya vikundi hivyo ili kuweza kutoa huduma ndani nan je ya Mkoa wa Rukwa.
Mtalitinya amesema kuwa miongoni mwa vikundi vilivyopewa mikopo hiyo kuna kinachojishughulisha na utengenezaji wa chaki, utengenezaji wa matofali, useremala na kufanya usafi hivyo aliagiza kuwa shule zote zilizopo chini ya Ofisi yake kuhakikisha wananunua chaki kutoka katika kiwanda hicho ili kukuza soko na mtaji wa kikundi hicho pamoja na kuvitumia vikundi vya usafi katika kushiriki kuiweka manispaa safi na kununua matofali kwaajili ya majengo ya taasisi za serikali katika vikundi hivyo.
“Kiwanda cha chaki ambacho tunakipa mkopo leo, tunaelekeza na ninaelekeza tena shule zangu zote za manipaa tutanunua chaki zote kutoka katika kiwanda hichi kama utekelezaji wa masoko, lakini pia kwa upande wa usafi hatutaajili wakala vikundi hivi vitapewa kazi kwaajili ya usafi, wapo wanaofanya kazi za useremala na kazi nyingine tutaendelea kuwatumia kwenye kazi zetu za ujenzi kama utengenezaji wa “Ma-grill” kuhakikisha wanapata ajira na masoko na mitaji yao iweze kukua,”Alisema.
Mtalitinya aliyasema hayo kwenye hafla fupi ya kukabidhi mikopo kwa vikundi 21 vya ujasiliamali iliyofanyika katika ukumbi wa manispaa ya sumbawanga ambapo mgeni rasmi wa hafla hiyo alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo.
Kwa upande wake Mh. Wangabo katika kuhakikisha masoko yanapatikana ndani ya mkoa aliziagiza halmashauri zote mkoani humo kuhakikisha wananunua chaki kutoka katika kiwanda cha kuzalisha chaki kilichopo manispaa ya sumbawanga ili kuthamnini na kukipa uwezo kikundi hicho kufanya vizuri na kukuza uzalishaji na kuongeza ajira.
“serikali yetu ya wamu ya tano inasisitiza uanzishwaji na uimarishwaji wa viwanda vyetu vya ndani ili tupunguze kuagiza kutoka nje, sasa kama taifa tunalenga hivyo mkoa na wenyewe uko hivyo hivyo, nilazima tuhakikishe kuwa bidhaa zetu za ndani tunapatia soko ndani hapa hapa na kwa hali hiyo hizi chaki tunazotengeneza wenyewe katika mkoa wetu ni lazima zitumike katika halmashauroi zetu zote,” Alibainisha.
Shilingi 70,590,000/= inatolewa leo hii ili kuwezesha Vikundi 21 vya ujasiliamali amba  13 ni vya Wanawake  7 vya Vijana na cha Walemavu.vikundi hivi  vinajishughulisha na Usindikaji mafuta, chakula,vinywaji, Useremala, Utengenezaji wa Chaki na ushonaji, ufumaji na utengenezaji wa Mabatiki na Ufugaji wa kuku na ngombe wa maziwa.

No comments:

Post a Comment