VODACOM FOUNDATION YADHAMINI PROGRAMU YA 'KUWA MJANJA' YA PSI - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Wednesday, 14 November 2018

VODACOM FOUNDATION YADHAMINI PROGRAMU YA 'KUWA MJANJA' YA PSI

Meneja ruzuku na mawasiliano wa Vodacom Tanzania Foundation,Sandra Oswald (katikati )  akiwa pamoja na wanafunzi  wa shule ya sekondari  Mbezi Mwisho jijini Dar es Salaam, wakielekezwa  na  mtaalam wa ubunifu wa kazi za mikono Flora  Richard   jinsi ya kutengeneza bangiri za batiki wakati wa Tamasha la Kuwa Mjanja  ambalo ni maalumu kwa ajili ya vijana kupata elimu ya Afya  iliyoandaliwa na PSI  kwa Udhamini wa Vodacom Tanzania Foundation.

Meneja ruzuku na mawasiliano wa Vodacom Tanzania Foundation,Sandra Oswald (watatu kushoto)   akionyeshwa    na  Meneja miradi wa PSI Tanzania, Dkt. Anna Temba  (wa pili kulia) ujumbe maalumu kwenye Tablet  ambayo ni maalumu kwa ajili ya kufundishia  elimu ya Afya kwa vijana  wakati wa tamasha la Kuwa Mjanja   lililofanyika katika shule yaSekondari Mbezi Mwisho jijini Dar es Salaam. Tamasha hilo ni maalumu kwa ajili ya vijana kupata elimu ya Afya  lililoandaliwa na PSI  kwa Udhamini wa Vodacom Tanzania Foundation. Kutoka  kushoto ni mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Goba  Magreth Richard, Agnes John, Mhamasishaji  wa Vijana PSI Semeni Likulo na Pendo Raphael (kulia).

Baadhi ya Wanafunzi wa shule ya sekondari Mbezi Mwisho jijini Dar es Salaam, wakijifunza elimu ya ujasiriamali wa kazi za mikono pamoja na Meneja Ruzuku na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Foundation, Sandra Oswald (Kulia) wakati wa tamasha la Kuwa Mjanja  ambalo ni maalumu kwa ajili ya vijana kupata elimu ya Afya, elimu ya ujasiriamali iliyoandaliwa na PSI kwa Udhamini wa Vodacom Tanzania Foundation. Tamasha hilo lilifanyika katika Viwanja vya shule ya msingi Mbezi Mwisho jijini Dar es Salaam.   

No comments:

Post a Comment