Na Mathias
Canal, Mtwara
WAZIRI wa Kilimo, Mhe Japhet Hasunga amesema kuwa wizara yake
itatekeleza maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dk. John
Pombe Magufuli kuhakikisha kuwa korosho yote inabanguliwa hapa nchini.
Ameyasema hayo jana tarehe 13 Novemba 2018 wakati akieleza malengo ya
ziara yake mkoani Mtwara na Lindi alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari
katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara kabla ya kuanza kukagua
maghala ya kuhifadhia korosho.
Hasunga alisema kuwa kuruhusu wafanyabiashara kubangulia nje ya nchi korosho
za wakulima wa Tanzania ajira nyingi zilikuwa zikipotea huku watanzania
wakisalia kuhangaika kutafuta ajira kwani ajira nyingi zilipelekwa nje ya nchi.
“Baada ya kujiridhisha tumeamua sasa hahutasafirisha korosho ghafi tunataka
korosho yote iwe inachakatwa nchini kwenye viwanda vyetu, kwa hiyo korosho zote
zilizokuwa zinachukuliwa na wafanyabiashara kwenda kubanguliwa sijui wapi huko
tumezuia” Alikaririwa Mhe Hasunga
Alisema kuwa viwanda vya kubangua korosho nchini vingi vimekufa kwa
sababu ya ubadhilifu wa wananchi wachache na baadhi ya hujuma za watu lakini serikali
imedhamiria kuanza kubangua kwenye viwanda vilivyopo kabla ya hatua za
kuanzisha viwanda vingi vya ubanguaji.
“Tunamuwezesha
mkulima kwa bei ya shilingi 3300 ili imsaidie kufanya kazi zake zingine ili
aweze kuongeza uzalishaji katika msimu ujao wa mwaka 2018/2019 na kuepuka
kushuka kwa uzalishaji” Alisisitiza Mhe Hasunga
Alisema
baada ya kukamilika uhakiki wa maghala yote ya kuhifadhia korosho serikali
itaanza kulipa malipo yote stahiki kwa wakulima yatakayotolewa na Benki ya
kilimo Tanzania (TADB).
“Na
tumeshaandaa fedha zao tunataka wakulima walipwe haraka iwezekanavyo lakini
tumeanza kumjali mkulima kwanza halafu taasisi zingine zinazofaidika na korosho
zitafuata” Alisisitiza
Mhe
Hasunga amewapongeza wakulima kwa kuwa wavumilivu katika kipindi hiki cha mpito
wakati serikali ilipokuwa ikitafuta ufumbuzi wa zao la korosho.
No comments:
Post a Comment