ARUSHA WATESA NAMTUMBO MARATHON, MSHINDI WA KWANZA KM 21 ATOKEA JKT - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Wednesday, 14 November 2018

ARUSHA WATESA NAMTUMBO MARATHON, MSHINDI WA KWANZA KM 21 ATOKEA JKT

Wanariadha mbalimbali walioshiriki namtumbo marathon wakichuana.


Mshindi wa kwanza wa kike KM21 Magdalena Crispin (katikati) baanda ya kukabidhiwa zawadi ya ushindi na Andrei Shutov (kulia) mwakilishi kutoka Uranium One  Urusi, wa pili kutoka kulia nimshindi wa pili Fabiola John na wa kwanza kushoto ni mshindi wa tatu Adelina Irasias.

MBIO za Namtumbo maarufu kama Namtumbo Selous Marathon zimefanyika mwishoni mwa wiki huko wilaya Namtumbo Mkoani Ruvuma ambapo mmoja kati ya wanaridha mbalimbali walijitokeza kushiriki katika mbio hizo Godfrey John Masaki kutoka JKT Arusha  aliibuka kidedea katika mbio za km21 kwa kushika nafasi ya kwanza na kumwacha, Mohamed Dule kutoka kikosi cha KG Songea akishika nafasi ya pili huku Ostin Kinyunyu kutoka Njombe akiibuka nafasi tatu.

Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo, Mh. Sophia Mfaume Kizigo akizungumza.


Akizumza na waandishi wa habari waliohudhuria katika tukio hilo Mkuu wa wilaya ya Namtumbo Mh. Sophia Mfaume Kizigo(Pichani) ambaye pia ni mshiriki wa mbio za KM 2.5 akivalia nambari 021 amewashukuru watanzania hasa wachezazji wa na washiriki wa mbio hizo kwa kujitokeza kwao kushiriki na kuhamasisha malengo yam bio hizo.

“Nashukuru mungu nimeweza kuwa mmoja wa washiriki wa mbio nimefanikiwa kumaliza  kilometa  mbili na nusu, nawashukuru sana washiriki na watanzania wote kwa kuja kutuunga mkono katika safari yetu ya kujenga maendeleo ya sekta ya afya” alisema mkuu huyo huku akipongeza jitihada za wadhamini wa mbio hizo Mantra Tanzania na Uranium One kwa ushirikiano mzuri wanaouonesha kwa wana namtumbo na watanzania kwa ujumla.

Kwa upande wake katibu wa afya wilaya ya Namtumbo Bw Yusuph Mwaipalu amesema sekta ya afya nchini na kote duniani na moja kati ya viungo muhimu sana katika ujenzi maendeleo ya kiuchumi katika jamii yoyote hivyo kuwaasa wana namtumbo na watanzania kwa ujumla kujenga tabia ya kujali afya zao kwanza ili kutengeneza taifa imara na yenye kujihami hapo baadae.

“Kwa niaba ya wana namtumbo na watanzania wote napenda kuwapongeza sana washiriki kwa kujitokeza kwa wingi lakini pia nawapongeza sekta zote husika kwa kujitokeza kushiriki katika harakati hizi ambazo lengo lake kubwa ni kuleta maendeleo chanya katika nchi yetu” alisema katibu huku akiwataka watanzani kujali mazoezi ya miili yao kama tiba ya kwanza. Mbio hizo zimepata kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa chama nawageni kutoka Urusi na mataifa mbalimbali duniani.


No comments:

Post a Comment