SPIKA NDUGAI AZUNGUMZA NA UGENI KUTOKA BENKI YA NMB - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Wednesday, 14 November 2018

SPIKA NDUGAI AZUNGUMZA NA UGENI KUTOKA BENKI YA NMB

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akizungumza na ugeni kutoka Benki ya NMB ulioongozwa na Ofisa Mkuu wa Mikopo wa Benki hiyo, Ndg. Tom Borghlos (wa pili kushoto) walipomtembelea leo tarehe 14 Novemba 2018 Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma. Wa tatu kushoto ni Mjumbe wa Bodi, Ndg. Jos Lange, Afisa wa Benki ya NMB, Ndg. Juliana muwanga (wa tatu kulia), Mkuu wa Biashara Benki ya NMB, Ndg. Donatus Richard (wa pili kulia) na Meneja kanda ya kati, Ndg. M. Nsolo.

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kulia) akiagana na Mjumbe wa Bodi wa Benki ya NMB, Ndg. Jos Lange pale ugeni kutoka Benki ya NMB ulipomtembelea leo tarehe 14 Novemba 2018 Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma. Kushoto ni Mkuu wa Biashara Benki ya NMB, Ndg. Donatus Richard.

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (watatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na ugeni kutoka Benki ya NMB ulioongozwa na Ofisa Mkuu wa Mikopo wa Benki hiyo, Bw. Tom Borghlos (watatu kulia) walipomtembelea leo tarehe 14 Novemba 2018 Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.(PICHA NA OFISI YA BUNGE).

No comments:

Post a Comment