MAADHIMISHO SIKU YA WAHANDISI TANZANIA YAINGIA SIKU YA PILI, MADA ANUAI ZAWASILISHWA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Thursday, 6 September 2018

MAADHIMISHO SIKU YA WAHANDISI TANZANIA YAINGIA SIKU YA PILI, MADA ANUAI ZAWASILISHWA

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari, Deusdedit Kakoko akiwasilisha mada kwa Wahandisi kwenye maadhimisho ya siku ya pili ya Siku ya Wahandisi Tanzania 2018 leo jijini Dar es Salaam.

Meza kuu katika uwasilishaji wa mada mbalimbali kwa wahandisi leo ikiwa ni siku ya pili ya Siku ya Wahandisi Tanzania 2018 leo jijini Dar es Salaam.

Sehemu ya wageni waalikwa na wahandisi mbalimbali wanaoshiriki katika hafla za Maadhimisho ya Siku ya Wahandisi Tanzania 2018 wakifuatilia majadiliano katika ukumbi wa Diamond Jubilee ikiwa ni sambamba na Bodi ya Usajili wa Wahandisi Tanzania kuadhimisha miaka 50 ya kuanzishwa Bodi hiyo leo jijini Dar es Salaam.

Kaimu Msajili wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi Tanzania, Injinia Patrick Barozi (wa kwanza kulia) pamoja na wageni anuai wakiwa katika majadiliano mara baada ya uwasilishwaji wa mada kwenye hafla ya Maadhimisho ya Siku ya Wahandisi Tanzania 2018 leo ikiwa ni siku ya pili ya maadhimisho yanayomalizika kesho.

Sehemu ya wageni waalikwa na wahandisi mbalimbali wanaoshiriki katika hafla za Maadhimisho ya Siku ya Wahandisi Tanzania 2018 wakifuatilia majadiliano katika ukumbi wa Diamond Jubilee ikiwa ni sambamba na Bodi ya Usajili wa Wahandisi Tanzania kuadhimisha miaka 50 ya kuanzishwa Bodi hiyo leo jijini Dar es Salaam.

Wahandisi wakijisajili katika banda la Bodi ya Usajili wa Wahandisi lililopo katika viwanja hivyo ili kushiriki siku ya pili ya maadhimisho ya Siku ya Wahandisi Tanzania 2018 leo jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya Wahandisi mbalimbali wakipata huduma za afya katika Kituo cha Moyo cha Jakaya Kikwete (JKCI), kinachoshiriki katika Maadhimisho ya Siku ya Wahandisi Tanzania 2018 leo jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya Wahandisi wakichangamkia huduma mbalimbali zinazotolewa na Banda la Shirika la Mawasiliano Tanzania, TTCL kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wahandisi Tanzania 2018 leo jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment