MATUKIO KATIKA PICHA BUNGENI DODOMA LEO SEPTEMBA 6, 2018 - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Thursday, 6 September 2018

MATUKIO KATIKA PICHA BUNGENI DODOMA LEO SEPTEMBA 6, 2018

Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe. Mussa  Sima akieleza mikakati ya Serikali kuhakikisha inatunza mazingira ya ziwa manyara ili kuondoa athari za mabadiliko ya tabia nchi.

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akisisitiza jambo wakati akijibu hoja za wabunge leo Bungeni Jijini Dodoma wakati wa kupitisha muswaada wa Sheria ya Bodi ya Taaluma ya Walimu Tanzania, 2018. (The Tanzania Teachers Professional Board Act, 2018).

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais , Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Geogre Mkuchika akieleza umuhimu wa muswaada wa Sheria ya Bodi ya Taaluma ya Walimu Tanzania, 2018. (The Tanzania Teachers Professional Board Act, 2018) wakati wa kupitishwa kwa muswaada huo leo Bungeni Jijini Dodoma.

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa Mhe. Rita Kabati akisisitiza kuhusu umuhimu wa wananchi kupata huduma bora za maji safi na salama wakati wa kipindi cha maswali na majibu leo Bungeni Jijini Dodoma.

No comments:

Post a Comment