Na Mwandishi Wetu
TAASISI ya Kimataifa ya Mikutano na Maonesho, NAMA International Conference and Exhibition - NICX inatarajia kufanya kongamano kubwa ambalo linalenga kuziunganisha asasi za kiraia kufanya kazi kwa ushirikiano zaidi kuongeza tija katika shughuli zao.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam na waandishi wa habari, Mratibu wa NICX kwa mwaka 2018, Bw. Shaban Mlongakweli amesema matarajio katika kongamano la mwaka huu ni pamoja na kuwatambulisha wataalamu kwenye nyanja za asasi za kiraia, elimu na maendeleo ya vijana.
Alisema kongamano la mwaka huu ambalo linatarajia kukusanya zaidi ya vijana 250 kutoka katika taasisi zaidi ya 100 litaitambulisha NAMA kama mbia wa maendeleo ambaye anafadhili na kuwaandaa wataalamu kutumika kwa ufanisi.
"NAMA Foundation ya Malaysia inaamini ufanisi wa asasi za kiraia unatokana na rasilimali zilizopo pamoja na elimu bora. Hivyo kuna wataalamu walioandaliwa kwenye nyanja mbalimbali za kiuongozi wa asasi kwenye maendeleo ya elimu na maendeleo ya vijana...pia NAMA tunaunga mkono juhudi za asasi za kiraia kwa kudhamini miradi mbalimbali za asasi hizo," alisema Bw. Mlongakweli.
Aidha aliongeza kuwa NAMA ina wataalamu wa ushauri, wabobezi wa elimu, wataalamu wa malezi kwa vijana pamoja na wataalamu wa kujitolea hivyo kuzitaka asasi za kiraia kujitokeza kwa wingi na kujadiliana kwa kina namna ya kuwatumia wataalam hao kwa maendeleo na pia kupanga namna bora ya ushirikiano utakaoleta tija kwa asasi hizo na taifa kwa ujumla.
Alibainisha kuwa kongamano hilo litakalofanyika Septemba 15, 2018, Serena Hotel ya jijini Dar es Salaam kwa siku moja kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa kumi na mbili jioni. Taasisi ya NAMA inafanya kazi kupitia washirika na kwa nchini Tanzania inajumuisha washirika An-Nahl Trust, Pamoja Foundation, TAMSYA, TAMPRO na UKUEM.
Hili si la kukosa kwa kweli
ReplyDeleteGreat Nama is one of the great partner of development of of our third sector organization as well as our Government now days
ReplyDeleteIs it open to all participants and what are the costs
ReplyDeleteFursa kubwa kwa Tanzania yetu...
ReplyDeleteAhsante sana Kwa maelezo mazuri na yenye kujitosheleza, Mungu awatie nguvu, awape baraka, jambo liende vizuri, In Shaa Allah.
ReplyDelete#NAMA FOUNDATION
#AN-NAHL TRUST