Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam, Bw. Badru
Idd (kulia) akimkabidhi viti 10 maalum vinavyotumika katika zoezi la
uchangiaaji damu Naibu Makamu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi
Muhimbili, na Mkuu wa Hospitali ya Taaluma na Tiba ya Mloganzila, Profesa Said
Aboud (kushoto). Viti hivyo vimetolewa na Wafanyakazi wa NMB Kanda ya Dar es
Salaam pamoja na kuchangia damu katika hospitali hiyo.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es
Salaam wakichangia damu ikiwa ni mchango wao kwa jamii.
Sehemu ya msaada wa viti 10 maalum vinavyotumika katika
zoezi la uchangiaaji damu vilivyotolewa na Wafanyakazi wa Benki ya NMB Kanda ya
Dar es Salaam katika zoezi la uchangiaji damu katika hospitali hiyo uliofanywa
na wafanyakazi hao.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es
Salaam wakichangia damu ikiwa ni mchango wao kwa jamii.
Sehemu ya Wafanyakazi wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es
Salaam wakipita kwa wataalam kutoka kitengo cha Damu Salama cha Hospitali ya
Taaluma na Tiba ya Mloganzila kabla ya kuchangia damu kwa wahitaji.
Sehemu ya Wafanyakazi wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es
Salaam wakipita kwa wataalam kutoka kitengo cha Damu Salama cha Hospitali ya
Taaluma na Tiba ya Mloganzila kabla ya kuchangia damu kwa wahitaji.
Naibu Makamu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi
Muhimbili, na Mkuu wa Hospitali ya Taaluma na Tiba ya Mloganzila, Profesa Said
Aboud (kushoto) akimshukuru Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam, Bw.
Badru Idd (kulia) mara baada ya kupokea msaada huo.
Na
Mwandishi Wetu
WAFANYAKAZI wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam mwishoni
mwa wiki wamefanya tukio lingine la kijamii kwa kwa kujitolea kuchangia damu kwa
lengo la kuwasaidia wagonjwa wahitaji.
Mbali na wafanyakazi hao kuchangia damu, wamejitolea michango
na kufanikisha kununua vitanda 10 maalum kwa ajili ya kuchangia damu, ambapo
kila kitanda kinagharimu kiasi cha shilingi 800,000 za Kitanzania na kuikabidhi
Hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi
Muhimbili, kilichopo Mloganzila, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa zoezi la kukabidhi msaada huo
pamoja na uchangiaji damu, Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam, Bw.
Badru Idd alisema wafanyakazi wameamua kujitoa kuchangia damu ili kunusuru
wagonjwa ambao wanaamini ni sehemu ya wateja wao.
Aliongeza kuwa mbali na kujitolea kuchangia damu pia
wafanyakazi hao wameguswa na kujichangisha na kununua vitanda 10 maalumu vinavyotumika
katika zoezi la kuchangia damu ili viwezekutumiwa na hospitali hiyo inayotoa
mchango mkubwa kwa jamii.
“Suala la kujitoa tumekuwa tukilifanya mara kwa mara
katika jamii yetu, lakini safari hii tulifikiria nini tukitoe kwa wananchi
ndipo tukaona kuna haja ya kujitoa na kuchangia damu kwa wagonjwa waitaji ili
kuweza kuokoa maisha yao.”
Anasema utaratibu wa kurejesha sehemu ya mapato kwa
wateja wao umekuwa ukifanywa pia na Benki kwa kujipangia kutoa sehemu ya
asilimia moja ya mapato ya kila mwaka na kuirejesha kwa jamii kupitia nyanja
mbalimbali.
Aidha alisema NMB imekuwa ikichangia jamii kwenye huduma
kama za afya, elimu, maji na huduma za msaada kwenye majanga yanapoikumba jamii
sehemu anuai nchini.
Anasema NMB itaendelea kujitolea kwa jamii pale
inapobidi, jambo ambalo imekuwa ikilifanya maeneo mbalimbali ya mikoa,
kulingana na ilivyojitanua katika utoaji huduma zake.
Kwa upande wake Naibu Makamu wa Chuo hicho-Huduma za
Hospitali ya Mloganzila, Profesa Said Aboud aliishukuru Benki ya NMB kwa msaada
huo na kuomba taasisi nyingine kuungana na benki hiyo kuiwezesha Hospitali ya
Taaluma na Tiba ya Mloganzila.
Alisema hospitali hiyo tangu kuanza kazi tayari
imehudumia zaidi ya wagonjwa 35,000 kutoka ndani na nje ya jiji la Dar es
Salaam, hivyo kuna kila sababu ya kuungwa mkono ili kukabiliana na changamoto
anuai katika kuhudumia wananchi.
Picha ya pamoja ya Wafanyakazi wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es
Salaam katika zoezi la uchangiaji damu.
No comments:
Post a Comment