Meneja wa Kituo cha Utafiti wa Mifugo (TALIRI) Kongwa Dodoma,Wilfredy Munisi akizungumza wakati wa utamburisho wa wagei waliofika katika kituo hicho kwa ajili ya hafla fupi ya utiaji saini katika makubaliano kati ya TALIRI na Taasisi Binafsi ya kusaidia Sekta ya Kilimo nchini ( PASS) ya kusaidia Wajasiliamali Vijana katika sekta ya Mifugo.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi Binafsi ya Kusaidia Sekta ya Kilimo nchini ,Nocomed Bohay (katikati) akizungumza wakati wa hafla fupi ya kutiliana saini kati ya Taasisi hiyo na TALIRI ya kusaidia Wajasiliamali vijana.Kulia ni Mkurugenzi wa Kituo cha Ubunifu katika Kilimo Biashara ,Tamim Amijee na kushoto ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo (TALIRI) Dkt Jonas Kizima.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi Binafsi ya Kusaidia Sekta ya Kilimo nchini ,Nocomed Bohay pamoja na Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo (TALIRI) Dkt Jonas Kizima wasaini Makubaliano kati ya Taasisi hizo mbili kusaidia Wajasiliamali vijana katika sekta ya Mifugo. Kulia ni Mkurugenzi wa Kituo cha Ubunifu katika Kilimo Biashara ,Tamim Amijee na kushoto ni Meneja wa Kituo cha Utafiti wa Mifugo Kongwa,Wilfredy Munisi.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi Binafsi ya Kusaidia Sekta ya Kilimo nchini ,Nocomed Bohay pamoja na Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo (TALIRI) Dkt Jonas Kizima wasaini Makubaliano kati ya Taasisi hizo mbili kusaidia Wajasiliamali vijana katika sekta ya Mifugo.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi Binafsi ya Kusaidia Sekta ya Kilimo nchini ,Nocomed Bohay wakibadilishana faili na Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo (TALIRI) Dkt Jonas Kizima zenye Makubaliano kati ya Taasisi hizo mbili kusaidia Wajasiliamali vijana katika sekta ya Mifugo.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi Binafsi ya Kusaidia Sekta ya Kilimo nchini ,Nocomed Bohay pamoja na Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo (TALIRI) Dkt Jonas Kizima wakionesha kwa wanahabari(hawako pichani) Makubaliano kati ya Taasisi hizo mbili kusaidia Wajasiliamali vijana katika sekta ya Mifugo.
Sehemu ya Mifugo (Mbuzi) inayofugwa katika kituo cha Utafiti wa Mifugo Kongwa.
PASS imejipanga kusaidia katika uwekezaji wa miundombinu ya ufugaji wa Mbuzi yakiwemo Mabanda ya Kisasa.
Mbuzi wakitoka katika Mabanda yao.
Ng'ombe wakiwa katika kituo cha utafiti wa Mifugo -Kongwa.
Mmoja wa watumshi katika kituo cha Utafiti wa Mifugo Kongwa akimlambisha Ndama vidole vyake.
Sehemu ya Mabanda ya mbuzi yaliyopo katika kituo hicho.
Na Dixon Busagaga, Dodoma
TAASISI ya Utafiti wa Mifugo (TALIRI) imetumia fursa ya mkoa wa Dodoma kuwa makao makuu ya nchi kuingia mashirikiano na Taasisi Binafsi ya kusaidia Sekta ya Kilimo nchini ( PASS) ya kuwekeza katika sekta ya Mifugo kwa kuwaandaa Wajasiliamali vijana.
Hatua hiyo inatajwa kuondoa moja ya changamoto ya upatikanaji wa bidhaa ya Nyama katika jiji la Dodoma ambalo kwa sasa idadi ya watu imeanza kuongezeka baada ya ofisi na taasisi mbaimbali za serikali na umma kuhamia Dodoma.
Akizungumza wakati wa hafla fupi ya utiaji saini makubalinao hayo iliyofanyika katika kituo cha Kongwa Dodoma ,Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi Binafsi ya kusaidia Sekta ya Kilimo Nchini(PASS) ,Nicomed Bohay alisema PASS kupitia kituo cha ubnifu wa Biasharaza Kilimo wameamua kuanzisha Vituo atamizi vya Mifugo katika kituo cha TALIRI Kongwa .
“Tumelenga kuanza na mifugo aina ya Mbuzi katika kituo hiki, zipo sababu zilizotupelekea tuweze kuchagua eneo hili la Kongwa moja wapo ni uwep wa soko la karibu ,… PASS tutawekeza kwenye Miundo mbinu ya ufugaji wa Mbuzi, pamoja na gharama za kuendesha mradi na malisho hadi mbuzi watakapo weza kuuzwa sokoni .”alisema Bohay .
Alisema kazi hiyo itafanyika kwa kutumia wajasiliamali Vijana wa Kitanzania na kwamba utaratibu wa kuwapata vijana wenye sifa utatangazwa baadae na watakao pata nafasi hiyo watapata nafasi ya kuunganishwa na taasisi za kifedha kwa ajili ya kupata mitaji.
“Kwa kuanza tumelenga kuanza na Unit 10 za mbuzi 100, kifupi tumepanga kuanza na Mbuzi 1000 kwa mwaka huu, nia yetu ni kwamba kutakuwa na Wajasiliamali vijana kama 20, ambao kila mmoja atakuwa na Mbuzi kama 50, na tutaongeza mbuzi 1000 kila mwaka hadi kufikia Mbuzi 5000 ndani ya kipindi cha miaka mitano ijayo.” alisema Bohay.
Bohay alisema kwa kuanzia PASS imetenga kiasi cha sh Mil 500, katika uwekezaji huo wa mwanzo kwa mifugo ya Mbuzi kutokana na uwepo wa gharama kubwa katika ujenzi wa miundombinu yakiwemo Mabanda ya kisasa.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo,Dkt Jonas Kizima alisema ujio wa PASS ni fursa muhimu kwa TALIRI kutumia utaalmau wa tafiti ili uweze kutumika na Wajasiliamali katika sekta ya Mifugo nchini.
“Kituo cha utafiti wa Mifugo ( TARIRI) kimesaini mkataba wa maelewano kwa ajili ya kuandaa wajasiliamali katika sekta ya mifugo ,kwetu sisi ni furaha inaipa nafasi sasa TALIRI ule ujuzi iliyonao ,zile Product ilizonazo ziweze kwenda sasa kwa wadau wengine kibiashara .”alisema Dkt Kizima.
Dkt Kizima aliyataja maeneo hayo kuwa sasa Taasisi hiyo ya serikali ambayo imejikita kwenye sekta ya mifugo itakuwa ni shamba darasa la kuwaandaa wajasiliamali ambao sasa watapata fursa ya kujifunza masuala mbalimbali yanayotolewa na TALIRI.
Alisema jambo jingine TALIRI itatoa Mbegu kwa ajili ya Malisho ya Mifugo na kwamba ujuzi utakaotolewa kwa wajasiliamali hao kwa kushirikiana na Taasisi ya PASS utasaidia upatikanaji wa Wajasiliamali Wasomi katika sekta ya Mifugo.
“Kitu kingine taasisi ya utafiti wa mifugo (TALIRI) itapata nafasi ya kuzitumia hizi takwimu za wajasiliamli kusambaza kwa wajasiliamli wengine nchini ili wazitumie waone wanaweza kufuga kibiashara kukuza uchumi wa nchi yetu,” alisema Dk. Kizima.
Taasisi ya utafiti wa Mifugo (TALIRI)ina vituo saba vilivyotengwa kikanda ambavyo ni TALIRI Kongwa - Dodoma, TALIRI West Kilimanjaro, TALIRI Tanga, TALIRI Naliendere Mtwara, TALIRI Uyole-Mbeya, TARILI Mpwapwa na TALIRI Mabuki, Mwanza.
No comments:
Post a Comment