ELIMU YA FEDHA YAFIKA MKOANI ARUSHA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Tuesday, 21 January 2025

ELIMU YA FEDHA YAFIKA MKOANI ARUSHA

 

Afisa Mwandamizi, Uchambuzi Fedha, Idara ya Sera, Utafiti na Mipango, kutoka Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), CPA. Gladness Mollel, akitoa elimu kwa wafanyabiashara na wajasiriamali wa Jiji la Arusha, kuhusu masuala ya uwekezaji.

Afisa Usimamizi wa Fedha kutoka, Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bw. Salim Khalfan Kimaro (wakwanza kulia) akimkabidhi Kaimu Katibu Tawala Msaidizi Mipango na Uratibu na Mtakwimu wa Mkoa wa Arusha Bw. Jonas Mwita, Nyenzo ya Kufundishia Elimu ya Fedha baada ya Timu hiyo ya kutoa elimu ya fedha kutoka Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kufika katika Ofisi yake jijini Arusha.

Afisa Usimamizi wa Fedha kutoka, Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bw. Salim Khalfan Kimaro, akizunguza katika Ofisi ya Kaimu Katibu Tawala Msaidizi, Mipango na Uratibu na Mtakwimu wa Mkoa wa Arusha, Bw. Jonas Mwita (hayupo pichani), baada ya kufika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha kabla ya kuanza kutoa elimu ya fedha katika mkoa huo.

Afisa Usimamizi wa Fedha kutoka, Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bw. Stanley Kibakaya, akizunguza katika Ofisi ya Kaimu Katibu Tawala Msaidizi, Mipango na Uratibu na Mtakwimu wa Mkoa wa Arusha Bw. Jonas Mwita (hayupo pichani),  baada ya kufika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha kabla ya kuanza kutoa elimu ya fedha katika mkoa huo.

No comments:

Post a Comment