NAIBU
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso akizungumza na wananchi wa
Kata ya Mkata wilayani Handeni wakati wa ziara yake ya kutembelea na
kukagua miradi ya Maji inayotekelezwa.
Mbunge wa Jimbo la Handeni Vijijini (CCM) Mboni Mhita akuzungumza katika ziaa hiyo.
MKUU
wa wilaya ya Handeni Godwin Gondwe katika akimueleza jambo Naibu Waziri
wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso kulia wakati wa ziara hiyo kushoto
ni Mkurugenzi wa Mtendaji wa wilaya ya Handeni William Makufwe.
NAIBU
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso kulia akimsikiliza kwa
umakini Mkuu wa wilaya ya Handeni Godwin Gondwe mara baada ya kutembelea
mradi wa Maji eneo la Mkata katikati ni Mkurugenzi wa Mtendaji wa
wilaya ya Handeni William Makufwe.
NAIBU
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso kulia akimsikiliza kwa
umakini Mbunge wa Jimbo la Handeni Vijijini (CCM) Mboni Mhita wakati wa
ziara hiyo kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Handeni Godwin Gondwe.
Wakandarasi ambao Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso aliotaka wawekwe ndani wakiwa chini ya ulinzi.
Naibu
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso wa pili kutoka kushoto akiwa
na Mkuu wa wilaya ya Handeni kulia wakati wakitembelea miradi ya maji
wilayani humo wakati wa ziara yake kulia ni Mkurugenzi wa Mtendaji wa
wilaya ya Handeni William Makufwe kushoto ni Diwani wa Kata ya Mkata.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso akiwa amepanda juu kwenye tenki eneo la mkata kulikagua wakati wa ziara yake.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso akiwa amepanda juu kwenye tenki eneo la mkata kulikagua wakati wa ziara yake.
Naibu
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso kushoto akilakiwa na
Mkurugenzi wa Mtendaji wa wilaya ya Handeni William Makufwe mara baada
ya kuwasili mjini Handeni.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso kulia akiwa na Mkuu wa wilaya ya Handeni Godwin Gondwe wakati wa ziara hiyo.
Mkurugenzi wa Mtendaji wa wilaya ya Handeni William Makufwe akimueleza
jambo Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso mara baada ya
kutembelea miradi ya maji kwenye eneo la Mkata katikati ni Mkuu wa
wilaya ya Handeni Godwin Gondwe akifuatilia kwa umakini.
Sehemu ya bwawa la maji lililopo eneo la Mkata wilayani Handeni.
NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso ameamuru kuwekwa ndani
wakandarasi wanaotekelezwa mradi wa maji yenye thamani ya zaidi ya
bilioni tatu eneo la mkata wilayani Handeni baada ya kushindwa kuwepo
kwenye eneo la mradi licha ya kupewa taarifa za uwepo wa ziara yake.
Wakandarasi ambao walilazimika kuwekwa ndani ni Mkandarasi wa Kampuni ya
Tansino Logistick Limited ya Dar Abdul Ismail na Charles Stephano
ambaye ni mkandarasi wa ujenzi huku Chales Tarimbo mshauri Mkandarasi
naye akikumbana na kadhia hiyo.
Agizo hilo alilitoa leo wakati wa ziara yake ya kutembelea na kukagua
miradi ya maji inayotekelezwa kwenye kata ya Mkata wilayani Handeni
ambapo miradi hiyo mitatu ilikuwa ikigharimu zaidi ya sh.bilioni tatu.
Akiwa kwenye eneo hilo Naibu Waziri huyo alisema haiwezekani wabunge
wanaomba miradi ya maji na serikali inatenga lakini watu wachache
wanatumia fedha hizo kwenye matumizi kwa maslahi yao binafasi na
kuwafanya wananchi kuendelea kuteseka na tatizo la maji.
Alisema kutokana na kuwepo kwa tabia hiyo ambayo imekuwa ikirudisha
nyuma juhudi kubwa zinazofanywa serikali hawatavumiliwa badala yake
watahakikisha wanachukuliwa hatua kali za kisheria ili kuweza kukomesha
vitendo vya namna hiyo kwenye jamii.
“Ndugu zangu wakati Rais akiniteua aliniagiza nihakikisha wananchi
wanapata 1maji vinginevyo nitatumbuliwaa nami sipo tayari kwa hilo hivyo
nitahakikisha tunawachukulia hatua kali wakandarasi wanaoshindwa
kuendena na kasi na hivyo kuikwamisha kwa maslahi yao binafasi huku
wananchi wakiendelea kuteseka”Alisema.
Naye kwa upande wake,Mbunge wa Jimbo la Handeni Vijijini (CCM) Mboni
Mhita alimuelezwa Naibu Waziri huyo kuwa mradi huo umejengwa chini ya
kiwango na kusababisha wananchi kuendelea kuteseka na adha ya maji.
“Mh Naibu Waziri wilaya ya Handeni ni miongoni mwa wilaya ambazo
zinachangamoto kubwa ya tatizo la maji lakini sisi kama wabunge tumekuwa
tukiiomba fedha za mradi ya maji lakini wakandarasi wamekuwa
wakitukwamisha”alisema.
Alisema kinachofanywa na wakandasi hao juu ya utekelezaji wa miradi hii
ni ubadhirifu wa wazi kabisa hivyo ili kuondokana na tatizo hilo
serikali inapaswa kuwachukulia hatua wakandarasi wa namna hiyo ili iwe
fundisho wa wengine wenye tabia za namna hiyo.
Naye kwa upande wake,Mkuu wa wilaya ya Handeni Godwin Gondwe alisema
miradi hiyo ambayo Rais aliagiza imalizike leo (jana)Julai 23 huku jambo
la kushangaza hakuna dalili ya umalizikaji wa miradi hiyo. Miradi hiyo
ambayo ilitakiwa kutelezwa Wilayani hapo ni pamoja na bwawa la
mkata,bwawa la manga na miundombinu ya mambomba toka katika bwawa la
mkata hadi mkata mjini jambo ambalo halijafanyika hadi mwisho wa agizo.
UBIA WA BARRICK NA TWIGA WACHOCHEA UTENGENEZAJI ENDELEVU WA THAMANI KATIKA
UCHUMI WA TANZANIA
-
Rais na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Barrick, Mark Bristow akizungumza katika
mkutano na waandishi wa habari
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kampuni ya ...
5 hours ago
No comments:
Post a Comment