Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita linamshikilia Jackline Peter, mkazi wa Mji Mdogo wa Katoro, Wilaya ya Geita, kwa tuhuma za kumshambulia kwa fimbo Rahel Jumanne, akimtuhumu kumuibia Shilingi 60,000.
Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Sophia Jongo, tukio hilo lilitokea Agosti 26, 2026, majira ya saa 5:00 asubuhi, katika nyumba ya mtuhumiwa iliyopo Katoro.
Alisema kabla ya tukio hilo, Jackline alidai kupoteza fedha hizo zilizokuwa kwenye pochi yake iliyokuwa chumbani, ndipo akaanza kumtilia shaka Rahel, ambaye alikuwa amemtembelea nyumbani kwake.
Alisema baada ya kubaini fedha hizo hazikuwepo, mtuhumiwa alimkamata Rahel na kuanza kumpiga kwa kutumia fimbo.
Wakati tukio hilo likiendelea, mtuhumiwa alimtaka mfanyakazi wake wa ndani kurekodi tukio hilo kwa kutumia simu yake, kabla ya baadaye kusambaza video hiyo kwenye mitandao ya kijamii.
Kamanda Jongo amesema Jeshi la Polisi lilipobaini video hiyo kwenye mitandao ya kijamii, lilianza ufuatiliaji na kufanikiwa kubaini eneo lilipotokea tukio, kumtambua mtuhumiwa na kumkamata.
Alisema mtuhumiwa anaendelea kuhojiwa wakati Jeshi la Polisi likikamilisha uchunguzi wa tukio hilo, na kwamba baada ya uchunguzi kukamilika atafikishwa katika mamlaka husika za kisheria kwa hatua zaidi.
Jeshi la Polisi limetoa wito kwa wananchi kuacha vitendo vya kujichukulia sheria mkononi na badala yake kutoa taarifa kwa mamlaka husika pale wanapodhani mtu amehusika na uhalifu.
-------------------------------------
𝗡𝗜𝗟𝗜𝗩𝗬𝗢𝗣𝗔𝗧𝗔 𝗠𝗧𝗢𝗧𝗢 𝗪𝗔 𝗞𝗜𝗞𝗘 𝗡𝗜𝗟𝗜𝗬𝗘𝗠𝗨𝗛𝗜𝗧𝗔𝗝𝗜 𝗕𝗔𝗔𝗗𝗔 𝗬𝗔 𝗠𝗜𝗔𝗞𝗔 𝗬𝗔 𝗞𝗨𝗧𝗔𝗙𝗨𝗧𝗔 𝗕𝗜𝗟𝗔 𝗠𝗔𝗙𝗔𝗡𝗜𝗞𝗜𝗢
Nilikuwa na ndoto moja kubwa moyoni kupata mtoto wa kike. Nilikuwa tayari nina watoto wa kiume, lakini tamaa yangu ya kuwa na binti haikutimia kwa miaka mingi. Kila nilipopata ujauzito, matumaini yangu yalikuwa makubwa. Lakini matokeo yalikuwa yale yale.
Nilianza kuchoka kihisia. Watu wengine walinicheka, wengine wakasema labda si majaliwa yangu. Nilijikuta nikiumia kimya kimya. Ilifika wakati nilianza kukata tamaa kabisa. Nilihisi kama ndoto yangu haitawahi kutimia. Siku moja nilikuwa nikiongea na dada yangu kuhusu hali yangu.




No comments:
Post a Comment