Mkurugenzi wa Shule za AFAP Juma Mti, akizungumza kwenye mahafali ya shule hiyo Septemba 1, 2026 wilayani Kisarawe mkoni Pwani.
NI nadra nyakati hizi watu wengi kuwajali yatima katika kuhakikisha nao wanapata elimu bora.
Hali tuliyonayo sasa hapa nchini mayatima na wale wanaotoka kwenye familia zenye kipato hafifu, wanafahamu kuwa kusoma katika shule za serikali ambazo hazina gharama kubwa ni haki yao kwa kuwa wazazi au walezi wao hawajiwezi kikipato.
Hali hiyo pamoja na mambo mengine inasababisha matabaka miongoni mwa familia za wenye nacho na wenye kidogo.
Wenye kipato cha kawaida na matajiri ambao wanaweza kugharamia ada kwenye shule za awali, msingi na sekondari ikiwamo cha msingi za mchepuo wa Kiingereza wanaona wao pekee wanastahili kusomesha watoto wao huko kwa sababu wanamudu gharama.
Licha ya kuwa jambo hilo linasababisha matabaka, lakini jambo la kufurahisha wanafunzi hao wanaosoma shule za serikali wakati mwingine katika mazingira magumu, wanasoma kwa bidii kubwa na kuwa na ufaulu mzuri katika mitihani yao ya mwisho
Hata hivyo, katikati ya mazingira wanayopitia watoto hao, mdau wa elimu Juma Mti yeye amejenga shule za awali, msingi na sekondari zinazojulika kama AFAP anawasomesha bure mayatima na kuwatoza ada nafuu watoto wa mama lishe na wale wanaouza mbogamboga.
Wazazi hao wanawakilisha wenzao wanauza vitumbua , karanga na hata wachoma mahindi mabichi barabarani.
Anasema shule zake za msingi zilizopo Kipawa na Mbondole jijini Dar es Salaam na ile ya bweni jwenye kijiji cha Msimbu Kisarawe, hiyo ni kuanzia awali. Msingi hadi sekondari.
Hata hivyo, mara kwa mara serikali inatoa matamko ya kuunga mkono jitihada mashirika ya dini, asasi za kiraia na watu binafsi wanaojenga mazingira bora ya kusomea ili kukuza kiwango cha elimu na ufaulu hapa nchini.
Wadau hao muhimu ambao shule zao nyingi za msingi zinafundisha kwa mchepuo wa lugha ya Kiingereza, ni pamoja na mashirika ya dini, watu binafsi na asasi za kiraia.
Shule hizo ambazo awali zilikuwa zimejengwa zaidi mijini, sasa wadau hao wameanza kuzisambaza hadi vijijini.
Hata hivyo, mara nyingi wanafunzi wanaosoma katika shule hizo ni wale wanaotoka kwenye familia zenye kipato nafuu.
Watoto wa mama na baba lishe, wauza samaki na mbogamboga mara nyingi ni ndoto kwao kupata elimu katika shule hizo kwa sababu zinatoza mamilioni ya shilingi.
Mkurugenzi wa Shule za AFAP, Juma Mti (kulia), akimuelekeza jambo Mkuu wa Shule ya Msingi na Sekondari ya Msimbu, wilayani Kisarawe, mkoani Pwani wakati wa mahafali yaliyofanyika Septemba 1, 2026.
.....................................................
Mkurugenzi wa shule hizo, Juma Mti anasema shule zake zimeanzishwa kusaidia watoto wanatoka mazingira magumu kwa ada nafuu huku mayatima wakisoma bure tangu shule ya chekechea.
"Ada kwa mwaka kwa shule za msingi kwa wanafunzi wanaokaa nyumbani ni sh. 600,000 na bweni sh. 1,320,000 kwa mwaka.
"Hata yule mwanafunzi ambaye anasoma hapa ikatokea baba yake anafariki dunia, atasoma bure," anasena Mti.
Mti ambaye kitaaluma ni mwalimu, anabainisha kuwa licha ya kuwa lengo kuanzishwa kwake ni kuwasaidia wenye kipato cha chini, wenye uwezo pia hawazuiwi kuwapeleka watoto wao katika shule hiyo.
Mdau huyo wa elimu anasema shule zake zinatoza ada inayolenga kuwawezesha familia za wazazi ambao wajasiriamali wadogo.
Anasema mtu mwingine akisikia kiasi cha ada chini ya milioni anadhani huenda elimu inayotolewa hapo ni hafifu, anasema ni sawa na bora kama wanaotoza mamilioni ya ada.
"Elimu inayotolewa hapa ni bora, na nidhamu kwa wanafunzi ni ya kupigiwa mfano,' anatanabahisha mti.
Anasema hilo linabainika kutokana na matokeo ya darasa la saba wanafunzi karibu wote kupata daraja la kwanza na wachache daraja la pili hakuna wa daraja la tatu, nne wala sifuri kwa darasa la Saba mwaka jana.
Siri ya kufanya vizuri darasani na nidhamu inatokana na watoto hao waliokutana kutoka familia tofauti wawapo shuleni hapo kupewa motisha na walimu na uongozi wa shule na hivyo kuwajenga katika ujasiri.
'Sisi huwa hatutumii viboko kwenye suala la nidhamu, tumewajenga katika misingi ya kidini zaidi na motisha kwa kutoa zawadi mbalimbali.
Kama mtoto wa Kikristo anakuja hapa hajapewa kipaimara, anafanyiwa mafundisho na kupewa sakramenti akiwa hapa, na watoto wa Kiislam wanasoma madrasa.
"Hata ninapofanya vikao na walimu mara nyingi nazungumzia kuhusu viboko, mwanafunzi kama amefanya vibaya safari hii, safari ijayo akiwa amejitahidi anapewa motisha inayomjenga na kumhamasisha asome vizuri na si mchapa," an
Anasema kwa yatima anayetaka kujiunga n shule hiyo anapewa fomu za kujaza na kuendelea na masomo yake bila malipo.
Mkuu wa Shule ya Sekondari wa shule hizo, akizungumza kwenye mahafali hayo.
.............................................
Akijibu kiwango kidogo cha ada kwa mwaka ikiwa kinakidhi mahitaji ya kuendesha shule hizo kwa maana ya kujenga madarasa, kulipa mishahara ya wafanyakazi na chakula.
"Kinachonisaidia mimi huwa sikopi kwenye mabenki, fedha ninazokusanya kutokana na ada zote naelekeza katika kulipa wafanyakazi na kuendeleza ujenzi wa majengo na huduma nyingine, ni bora nibaki bila fedha kuliko wafanyakazi wangu wasilipwe ," anasema Mkurugenzi Mti.
Akifafanua kuhusu shule zake anasema wazo la kuanzishwa kwake alikuwa na hamu kubwa ya kumpeleka katika shule za mchepuo wa Kiingereza binti yake lakini alishindwa kutokana na kipato duni alichokuwa nacho mwanzoni mwa miaka ya 2000.
Hata hivyo, baadaye akaona aanzishe masomom ya ziada nyumbani kwake ambapo alikuwa akifundisha na mke wake kwa lugha ya Kiingereza, kulikuwa na mwitikio mkubwa wa wanafunzi hivyo akaona aanzishe shule ya Kwanza Kipawa baadaye Msimbu Kisarawe na Mbondole.
Mti anatanabahisha kuwa kipato kidogo kinachopatikana kwa ajili ya kuendeleza shule hiyo hata ikiwa kuna wafadhili wanaguswa kumpa ufadhili yupo tayari kwa sababu yatima walioko ni wengi ambao wanasomeshwa hapo tangu chekechea hadi sekondari.
Anasema kutokana na kufanya kazi na mashirika mbalimbali ndipo alibaini jamii kubwa inapitia changamoto za kimaisha zinazotokana na kipato duni.
Hivyo, akaona anzishe shule hiyo huku msukumo mkubwa ulilenga kuwasaidia wenye kipato duni nao waone fahari kupata elimu bora kutokana na kipato cha chini cha wazazi wao.
Anasema AFAP Kisarawe ambayo ipo katika kijiji cha Msimbu, ndiyo ya bweni na ina wanafunzi kuanzia chekechea hadi kidato cha pili huku lengo ni kuwa na hadi chuo kikuu.
Anabainisha kuwa wazazi na walezi wasisite kuwaleta watoto wao shuleni hapo kwani watapata elimu bora na nidhamu njema ya kupigiwa mafano.
Vyeti vikikabidhiwa kwa wahitimu.
........................................
Wazazi wengi wanashangazwa na mabadiliko ya tabia ya watoto wao baada kuanza shule katika shule zetu, wanakuwa watulivu wasio na papara za kutembea huku na huko.
Anasema shule za Kipawa na Mbondole ni za kutwa na mwisho ni darasa la saba licha ya kuwa mchakato ni kuanza kujenga madarasa ya sekondari.
Licha mafanikio anayojivua kwa shule zake, Mti anasema changamoto zinazomkabili ni pamoja na wazazi na walezi kutolipa ada kwa wakati, hivyo anawakumbusha kuonesha ushirikiano mzuri zaidi na shule ikiwa ni pamoja na kulipa ada kwa wakati hatua ambayo itaisaidia menejimenti kuendesha shughuli zake kwa ufanisi mkubwa.
Pia shule ya Msimbu inakabiliwa na tatizo la ukosefu wa umeme ambapo analazimika kutumia chanzo cha umeme jua kwa gharama kubwa ili kukidhi mahitaji makubwa ya mwanga na katika maabara.
Anasema amejitahidi sana kufuatilia suala la kuletewa umeme lakini limegonga mwamba.
Anaiomba Serikali kupeleka umeme katika shule yake ya Msimbu ambao ni muhimu mno ikiwapo katika kuleta mwaka na matumizi ya maabara za shule hiyo.
Salamu zikitolewa kwenye mahafali hayo.
Wanafunzi wakitoa burudani za kitaaluma wakati wa mahafali hayo.
Burudani zikiendelea.
Burudani zikitolewa na wanafunzi wa shule hiyo.
Igizo likioneshwa kwenye mahafali hayo.
Walimu wakitoa salamu kwenye mahafali hayo.
Taarifa zikitolewa kwenye mahafali hayo.
Walimu wakijitambulisha kwenye mahafali hayo.
Mkurugenzi wa Shule za AFAP Juma Mti (kulia), akisalimiana na washiriki wa mahafali hayo.
Wanafunzi waa shule hiyo wakitoa burudani za kitaaluma kwenye mahafali hayo.
Walimu wa shule zinazomilikiwa na Kampuni ya AFAP wakiwa katika picha ya pamoja.
......................................
Makala hii imeandaliwa na Claudia Kayombo namba ya Simu 0713144299.


















No comments:
Post a Comment