MFUKO wa Kusaidia Elimu katika Halmashauri ya Wilaya ya Itigi mkoani Singida unatarajia kuanzishwa baada ya Diwani wa Kata ya Itigi Mjini Ally Minja kuandika andiko na kulipeleka kwa madiwani na kupokelewa kwa mikono miwili.
Akizungumza
kwenye kikao cha Baraza la Madiwani lililoketi Agosti 12, 2026 kwa lengo la
kupokea, kupitia na kujadili taarifa za utekelezaji wa miradi mbalimbali ya
maendeleo (ikiwemo miundombinu, afya, elimu na maji) kwa mwaka wa fedha
2025/2026, Makamu Mwenyekiti wa Halmshauri ya Wilaya ya Itigi, Mhe. William
Lupaa alisema wazo hilo limepokelewa kwa mikono miwili na Madiwani.
“ Wazo hili kupitia andiko la Mhe. Ally Minja Diwani wa Kata ya Itigi Mjini ni zuri na tumelipokea kwa mikono miwili lakini tumelipeleka kwenye Kamati ya Elimu na Afya ili likajadiliwe na kuona hatua nyingine zitakazo fuata,” alisema Lupaa.
Akizungumzia
manufaa ya mfuko huo Mhe Minja alisema suluhisho la pamoja aliloliona hadi
kufikia tafakari hiyo ni kuiomba Halmashari ya Wilaya ya Itigi kuanzisha Mfuko
wa Elimu kwa ajili ya kukusanya rasilimali fedha kutoka maeneo mbalimbali.
“Fedha zitakazopatikana zitawasaidia watoto na kizazi chetu kiweze kupata elimu,” alisema Minja.
Minja
alisema ikumbukwe kwamba kipaumbele cha elimu ni kikubwa kuliko vingine vyote
na ndiyo urithi mkubwa ambao ni miongoni na ule watakao achiwa.
Akielzea namna ya kupata fedha hizo ni pamoja
na kuanzisha uhamasishaji wa upatikanaji wa fedha ya kusomesha watoto wetu na
njia bora nyingine za kupata fedha hizo.
Akitolea
mfano mwingine alisema “Agosti 11 katika halmashauri hiyo ulifanyika mnada wa
kuuza kilo milioni 2.5 za dengu ambapo kama tukiwaomba wakulima kupitia vyama
vyao angalau shilingi 10 tu kwenye kila
kilo ambayo inaweza kuonekana haina kazi
lakini kwa mnada huo uliofanyika wangeweza kupata shilingi milioni 25.
“Kwa mnada wa jana tu tunge weza kupa kiasi hicho cha fedha ambazo zingeingia kwenye mfuko huo na mpaka minada mingine ije imalize msimu ingekuwa tumepata shilingi ngapi,” alihoji Minja.
Aidha, Minja
alisema hiyo ni kwa zao la ndengu je wakienda kwenye zao la pamba ambalo
linauzwa kwa ushirika ambayo inalimwa kwenye vijiji vya Kitaraka, Lyandole na
kata nyinge hapo hawajaenda kwenye zao la tumbaku na kupata michango kutoka taasisi
mbalimbali na Asasi nyingine kuchangia elimu.
Minja aliongeza kuwa hilo wazo linaweza kuonekana la kawaida kwa sasa kwa sababu baadhi ya watu wamezoea kuweka ubinafsi mbele lakini shida ya mtoto kukosa fedha za kumuendeleza kusoma shule linaikumba kila nyumba.
Alisema hali hiyo ni kama ilivyo kwa
maradhi na katika ukoo ambao haujawahi kukumbwa na changamoto ya mtoto
kushindwa kuendelea na masomo kwa kukosa rasilimali fedha hivyo halmashauri
hiyo ikianzisha mfuko huo itaweza kusaidia watoto kwa mamia kuweza kuendelea na
masomo ambao utakuwa msaada mkubwa sana.
Makamu Mwenyekiti wa Halmshauri ya Wilaya ya Itigi, Mhe. William Lupaa (katikati) akiongoza Baraza la Madiwani lililoketi Agosti 12, 2026 mkoani Singida. Kutoka Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Ayubu Kambi, Kaimu Katibu Tawala wa wilaya hiyo Charles Magesa na Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya yaa Manyoni na Itigi, Maimuna Makunguni.

No comments:
Post a Comment