MAHITAJI YA KOROSHO GHAFI YA VIWANDA YATAONGEZA UZALISHAJI - THE HABARII

THE HABARII

HABARI | MATUKIO | MICHEZO.


ASAS GROUP

Habari Mpya


Thursday, 6 August 2026

MAHITAJI YA KOROSHO GHAFI YA VIWANDA YATAONGEZA UZALISHAJI

Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Dk. Fatuma Mganga ambaye alikuwa mgeni rasmi Siku ya Korosho wakati wa Maonesho ya Wakulima Nanenane  na Maadhimisho  miaka 10 ya Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) yaliyofanyika Uwanja wa Maonesho wa Dk. John Malecela Jijini Dodoma akihutubia Agosti 6, 2026. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu TARI, Thomas Bwana na kulia ni Mkurugenzi wa Masoko na Udhibiti Ubora wa Bodi ya Korosho Tanzania (CBT), Hamidu Mponda.

................................

Na Dotto Mwaibale, Dodoma

MAHITAJI makubwa ya korosho ghafi kwa ajili ya viwanda yataongeza uzalishaji na kusaidia kufikia lengo la Serikali la kuzalisha tani milioni moja za korosho katika msimu wa 2026/2027.

Hayo yamebainishwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida, Dk. Fatuma Mganga ambaye alikuwa mgeni rasmi Siku ya Korosho wakati wa Maonesho ya Wakulima Nanenane  na Maadhimisho  miaka 10 ya Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) yaliyofanyika Uwanja wa Maonesho wa Dk. John Malecela Jijini Dodoma Agosti 6, 2026.

“ Tayari tunaona mafanikio ya zao hilo ambapo uzalishaji umeongezeka na kufikia tani 618,497 katika msimu wa 2025/2026,” alisema Dk. Mganga.

Alisema pamoja na mafanikio hayo, bado kuna kazi kubwa ya kufanya katika uchakataji wa korosho.

Alisema hivi sasa chini ya asilimia 20 ya korosho zinazozalishwa hubanguliwa hapa nchini, huku zaidi ya asilimia 80 zikiuzwa kama korosho ghafi.

Dk. Mganga aliongeza kuwa ni matarajio ya Serikali kuona kiwango cha ubanguaji wa ndani kinaongezeka na kufikia angalau asilimia 60 ifikapo mwaka 2029/2030.

Alisema Kaulimbiu ya Maonesho ya Nanenane ya mwaka huu inasema:"Tambua Soko, Zalisha kwa Tija Kutekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050."

Alisema Kaulimbiu hiyo inatukumbusha kuwa mafanikio ya kilimo yanategemea uzalishaji wenye tija unaoendana na mahitaji ya soko.

 “Hivyo, naiomba TARI iendelee kufanya utafiti unaochochea ubunifu na uongezaji thamani wa zao la korosho, huku Bodi ya Korosho ikiendelea kuhamasisha matumizi ya korosho na bidhaa zake nchini,”.  alisema Dk.Mganga.

Aidha, aliiomba Bodi ya Korosho na TARI kuhakikisha kuwa Siku ya Ulaji wa Korosho inaendelea kuadhimishwa kila mwaka ili kuimarisha uelewa wa wananchi na kuongeza matumizi ya zao hilo muhimu.

“ Maadhimisho ya Siku ya Ulaji wa Korosho na bidhaa zake, yamelenga kuhamasisha matumizi ya korosho zinazozalishwa hapa nchini na kuongeza uelewa wa wananchi kuhusu mchango wake katika afya, uchumi na maendeleo ya Taifa,” alisema.

Dk. Mganga alitumia nafasi hiyo kutoa rai kwa wananchi wote kuendelea kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya uongozi wa Dk. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye ameendelea kuweka mazingira bora ya maendeleo ya sekta ya korosho kupitia uwekezaji katika utafiti, upatikanaji wa pembejeo, hususan viuatilifu vya bure, pamoja na sera mbalimbali zinazolenga kuongeza tija na kipato cha wakulima..

Mkurugenzi wa Masoko na Udhibiti Ubora wa Bodi ya Korosho Tanzania (CBT), Hamidu Mponda ambaye alimwakilisha  wa bodi hiyo Francis Alfred alisema zao hilo limekuwa likiongezeka kutoka tani 210,000 msimu wa 2021/2022 ambapo msimu wa 2025/2026 wameweza kuzalisha tani 618,000 wakiwa na lengo la kuzalisha tani milioni moja ifikapo mwaka 2030.

Aliongeza kuwa kutokana na mafanikio makubwa waliyopata upande wa uzalishaji wameamua kuelekeza nguvu zao kuongeza thamani ya zao hilo.

Alisema kimsingi pamoja na zao hilo kuleta tija kwa wakulima, kuongeza mapato kwa Serikali halitoi tija kubwa kama wataendelea kuuza korosho ghafi,  kwenye msimu waliouza tani 618,000 tani 439,000  ziliuzwa nje ya nchi kama korosho ghafi jambo ambalo linapoteza ajira, na faida za kikodi ambazo Serikali ingepata .

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TARI Thomas Bwana alisema dira ya 2050 inataka tufikie uchumi wa juu, kati na kuwa hatuwezi kufikia hatua hiyo pasipo uchumi wa wananchi kukua kwani tunategemea uchumi wa kilimo ambao hauwezi kukua bila kilimo kukua.

“Kilimo kinategemea ongezeko la tija na jambo hilo litakuwa na tija iwapo tu zitatumika teknolojia sahihi ambazo zinatoka kwenye utafiti ambao ndiyo roho ya dira na ndiyo maana watafiti wanafanya kazi kuhakikisha wananchi wanapata teknolojia sahihi na kuongeza uzalishaji, wapate tija hili uchumi wao uongezeko kufikia malengo ya dira.

Mkurugenzi Mkuu TARI, Thomas Bwana, akizungumza.
Mkurugenzi  Uhaulisha wa Teknolojia TARI, Dk. Sophia Kashenge akizungumza.

  Mkurugenzi wa Masoko na Udhibiti Ubora wa Bodi ya Korosho Tanzania (CBT), Hamidu Mponda ambaye alimwakilisha Mkurugenzi wa bodi hiyo Francis Alfred, akitoa salamu za bodi hiyo.

Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Dk. Fatuma Mganga, akihutubia 
Viongozi wa TARI wakiwa kwenye Maadhimisho hayo. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Kituo TARI Selian Arusha, Mkurugenzi wa Kituo TARI Mlingano Tanga, Dk. Mgeta Merumba, Meneja wa Kituo TARI Dakawa Morogoro, Dk. Jerome Mghase, Meneja waa Kituo TARI Kibaha Dk. Nessie Luambano na Meneja waa TAARI Tengeru Dk. Happyness Gabriel.
Watafiti Grace Masalu kutoka TARI Ukiriguru na Happiness Mnanka kutoka TARI Ilonga wakiwa kwenye Maadhimisho hayo.

Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Dk. Fatuma Mganga ambaye alikuwa mgeni rasmi akinywa maziwa yaliyotokana na korosho.
Mkurugenzi Mkuu TARI, Thomas Bwana, akila andazi lililotokana na korosho.
Mkurugenzi  Uhalisha wa Teknolojia TARI, Dk. Sophia Kashenge akila andazi lililotokana na korosho.
Wafanyakazi wa TARI na Wageni waalikwa wakiwa katika foleni ya kwenda kupata bidhaa zinazotokana na korosho kama vile maziwa ya korosho, maandazi ya korosho, korosho, mvinyo wa korosho na nyinginezo.

Maadhimisho hayo yakiendelea.
Maadhimisho yakiendelea
Mkurugenzi Miss Korosho Mkoa wa Dodoma, Alex Nikijaz (kulia), na Angela Mndolwa (katikati na Martha Natumwa ambao ni wageni waalikwa kutoka Hospitali ya Taifa (MNH), wakiwa kwenye Maadhimisho hayo.

Mgeni rasmi Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Dk.Fatuma Mganga akiangaliaaa bidhaa mbalimbali zinazotokana na korosho.
Viongozi wa TARI wakila bidhaa zinazotokana na korosho.
Wageni waalikwa na Wafanyakazi wa TARI wakipata bidhaa zilizotokana na korosho.
Wanamuziki kutoka Bendi ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT),  Makutopora wakitoa burudani kwenye Maadhimisho hayo.

Habari hii imeandaliwa na Dotto Mwaibale simu namba 0754362990. 

No comments:

Post a Comment