SERIKALI INA WAJIBU WA KUTENGENEZA MAZINGIRA RAFIKI YA MTANZANIA - THE HABARII

THE HABARII

HABARI | MATUKIO | MICHEZO.


ASAS GROUP

Habari Mpya


Friday, 7 August 2026

SERIKALI INA WAJIBU WA KUTENGENEZA MAZINGIRA RAFIKI YA MTANZANIA

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dennis Londo, akizungumza na waandishi wa habari alipotembelea Banda la Wizara ya Viwanda na Biashara katika Maonesho ya Wakulima Nanenane Kitaifa 2026 yanayofanyika Viwanja vya Dk. John Malecela Jijini Dodoma Agosti 7, 2026. 

SERIKALI inawajibu wa kumtengenezea mazingira rafiki Mtanzania ili kumurahisishia shughuli zake za kiuchumi.

Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dennis Londo, wakati akizungumza na waandishi wa habari alipotembelea Banda la Wizara ya Viwanda na Biashara katika Maonesho ya Wakulima Nanenane Kitaifa 2026 yanayofanyika Viwanja vya Dk. John Malecela Jijini Dodoma Agosti 7, 2026.

“ Kila Mtanzania anapaswa kutengenezewa mazingira rafiki awe mkulima, mfugaji na mvuvi,” alisema  Mhe. Londo.

Mhe. Londo aliongeza kusema kuwa mwananchi anapopunguziwa gharama hizo anakuwa na uhakika wa kuzalisha kwa tija na kuwa na uhakika wa kuwa na akiba ya chakula cha kutosha.

Aidha, Naibu Waziri Londo alisema Serikali inachokifanya ni kujenga barabara, vivuko na madaraja ili kumuwezesha mkulima kutoka mashambani kwenda kwenye masoko na  viwandani.

Alisema Serikali hivi sasa inaendelea kusambaza umeme kupitia Wakala wa Umeme Vijijini (REA) katika vijiji  na vitongoji vyote ili kumpunguzia gharama mwananchi za uzalishaji.

Habari hii imeandikwa na Dotto Mwaibale namba ya simu 0754362990. 

No comments:

Post a Comment