Afisa Biashara wa Halmahauri ya Wilaya ya Itigi mkoani Singida, Richard Mmuni katika Maonesho ya Wakulima Nanenane Kitaifa 2026 yanayo endelea Uwanja wa Maonesho wa Dk. John Samuel Malecela Jijini Dodoma Agosti 7, 2026.
........................
HALMASHAAURI
ya Wilaya ya Itigi mkoani Singida inajivunia mafanikio makubwa tangu ianze
kushiriki Maonesho ya Wakulima Nanenane Kitaifa sasa ikiwa ni miaka 9
inashiriki.
Hayo yameelezwa na Afisa Biashara wa Halmahauri hiyo, Richard Mmuni katika Maonesho ya Wakulima Nanenane Kitaifa 2026 yanayo endelea Uwanja wa Maonesho wa Dk. John Samuel Malecela Jijini Dodoma Agosti 7, 2026.
“Ushiriki wa Halmashauri yetu katika maonesho haya kumekuwa na tija kubwa hasa kutangaza fursa mbalimbali zinazopatikana kwenye sekta mbalimbali,” alisema Mmuni.
Awali ya
yote Mmuni ameipongeza Serikali chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fursa ya kuandaa Maonesho hayo
ambayo ni ya muhimu kwa taifa hasa wakati huu ambao sekta ya kilimo inapewa
nafasi kubwa katika kuchangia pato la taifa.
Mmuni alisema katika Halmashauri ya Wilaya ya Itigi ina fursa mbalimbali
inayoshughulika nazo ikiwemo sekta ya kilimo.
“ Halmashauri yetu ni kinara kwa kilimo cha dengu kwa msimu uliopita tulifanikiwa kuuza tani 17,207 na baada ya kuziuza tulipata jumla ya Shilingi bilioni 19 ambazo zilienda kwa wakulima na kuinua uchumi wao kutoka wa chini kwenda juu,” alisema Mmuni.
Mmuni alitumia nafasi hiyo kuwakaribisha wawekezaji, wakulima na wafanyabiashara kwenda katika wilaya hiyo kuwekeza kwani bado
wana maeneo ya kutosha kwa kilimo cha dengu ambalo ni zao zuri na linaongeza
thamani na uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.
Mmuni alisema kuwa pia halmashauri hiyo kutokana na kuwa na misitu mikubwa pia
inajishughulisha na ufugaji wa nyuki na kupatikana kwa mazao yake kama asali
yenye ubora wa juu.
Aliongeza
kusema kuwa katika halmashauri hiyo inavikundi 11 vya ujasiriamali ambavyo
vinajishughulisha na mazao yanayotokana
na nyuki.
Alisema wana
mizinga 42 ya kisasa na mizinga 85 ya
kienyeji ambayo imesambazwa katika misitu mbalimbali iliyopo kwenye halmashauri
hiyo.
“Katika Maonesho haya ya wakulima hapa Dodoma tumekuja na asali yetu nzuri hivyo tunawakarisha wananchi na wadau mbalimbali kufika kwenye banda letu kuona na kununua bidhaa mbalimbaali zinazotokana na nyuki,” alisema Mmuni.
Aidha, Mmuni alisema kuwa katika halmashauri yao inajishughulisha na ufugaji wa
ng’ombe, mbuzi na kuku.
Alisema
katika eneo la kilimo pia wanalima zao la alizeti ambalo linatoa mafuta
yanayofaa kwa afya ya binadamu na mashudu ambapo anawahamasisha wawekezaji
kwenda kulima zao hilo.
Katika
Maonesho hayo wamefika na bidhaa mbalimbali zinazotokana na shughuli
wanazozifanya katika Halmahauri ya Wilaya ya Itigi, kama unga waa dengu, mafuta
ya alizeti na zile zinazotokana na nyuki hivyo anawakaribisha wananchi kufika
katika banda lao kujipatia kwa bei nzuri kabisa.
Mmoja wa Wananchi akihudumiwa alipotembelea Banda la Halmashauri ya Wilaya ya Itigi katika Maonesho hayo.
Habari hii imeandaliwa na Dotto Mwaibale namba ya simu 0754362990.

No comments:
Post a Comment