RAIS SAMIA AWAAPISHA VIONGOZI MBALIMBALI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Saturday, 24 May 2025

RAIS SAMIA AWAAPISHA VIONGOZI MBALIMBALI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Prof. Tumaini Joseph Nagu kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia masuala ya Afya kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 24 Mei, 2025.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Dkt. Blandina Bugazi Kilama kuwa Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango anayeshughulikia biashara na ubunifu kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 24 Mei, 2025.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Jaji Mstaafu John Samweli Mgetta kuwa Mjumbe wa Baraza la Maadili kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 24 Mei, 2025.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi mara baada ya tukio la uapisho Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 24 Mei, 2025.

Viongozi wateule wakiapa Kiapo cha Maadili kwenye hafla ya uapisho iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 24 Mei, 2025.

Viongozi wateule wakiapa Kiapo cha Maadili kwenye hafla ya uapisho iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 24 Mei, 2025.


 Viongozi wateule wakisaini viapo vya Maadili.

No comments:

Post a Comment