Mtoto Abubakar Tenda (10) anayesumbuliwa na maradhi ya pumu ya ngozi na moyo kwa zaidi ya miaka tisa.
Na Dotto
Mwaibale
LATIFA Saidi
(37) mkazi wa Mtoni Mtongani Mtaa wa Mseti Temeke Jijini Dar es Salaam
anawaomba wadau mbalimbali kumsadia kupata
Sh. Milioni 3.2 kwa ajili ya matibabu ya mtoto wake Abubakar Rajabu
Tenda (10) anayesumbuliwa na maradhi ya pumu ya ngozi na moyo kwa zaidi ya
miaka tisa.
Mama huyo
anasema alimzaa Abubakar Juni 10, 2014 Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke
Jijini Dar es Salaam akiwa na kilo 4.5 jambo ambalo liliwashitua hata wauguzi
waliokuwa wakimuhudumia.
Anasema
alianza kuona mabadiliko ya mtoto huyo alipofikisha miaka mitatu kwani ngozi
yake ilianza kuonesha kutokwa na upele ndipo alipo mpeleka Hospitali ya kwa
Bruda iliyopo Kijijichi lakini hakupata nafuu.
Latifa
anasema aliendelea kumtibu katika hospitali mbalimbali na alipofikisha miaka
sita akawa anapata joto kali nyakati za usiku, kukooa sana na uso kuvimba ndipo
alipompeleka tena Hospitali ya Temekea ambapo walimuambia kuwa alikuwa na
changamoto ya moyo hivyo ampeleke Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) kwa
ajili ya matibabu.
Alisema
baada ya kufanyiwa vipimo alielezwa kuwa moyo wake umetanuka hivyo anatakiwa
kufanyiwa upasuaji kwa gharama ya fedha Sh. Milioni 3.2 fedha ambazo ameshindwa
kuzipata jambo linalomfanya mtoto wake huyo aendelee kuteseka na kushindwa
kuanza shule.
“Kwa kweli
sijui hatima ya mwanangu kwani wakati wote hana furaha na sijui nitapata wapi
hizo fedha sina kazi zaidi ya kuuza vijiazi hapo epenuni kwa nyumba ya jirani
na mume wangu naye hana kazi ya uhakika hivyo kutuwia vigumu namna ya kupata
fedha hizo,” alisema Latifa.
Alisema
mwezi uliopita ndio ilikuwa ampeleke kliniki lakini hadi leo hii ameshindwa
kufanya hivyo kwani kila inapofika tarehe ya kliniki anatakiwa awe na Sh.
120,000 kwa ajili ya vipimo na mahitaji mengine ya chakula, na usafiri fedha
ambayo hana kwani hatakodi ya nyumba ambayo ni zaidi ya Sh.250,000 ameshindwa
kulipa.
“Kwa kweli
sina mbele wala nyuma sijui nitazimaliza vipi hizi changamoto nilizonazo nawaombeni
watanzania wenzangu kwa nafasi zenu mlizojaaliwa na Mwenyezi Mungu mnisaidie
hasa fedha na matibabu ya mtoto wangu ambaye anapenda kusoma lakini ndio hivyo
tena maradhi yanamsumbua,” alisema Latifa huku akitokwa na machozi na kuonesha
kukata tamaa.
Mjumbe wa
Serikali ya Mtaa wa Mianzini Maji Matitu 'A' Mbagala kupitia Chama Cha
Mapinduzi (CCM), Hawa Omari ambaye amemuibua mtoto huyo ameiomba jamii na
watanzania kwa ujumla kuungana kwa kufanya vitendo vya huruma kwa makundi
mbalimbali ya wenye uhitaji na changamoto za aina tofautitofauti jambo
litakalosaidia kuwa na taifa lenye upendo badala ya kusubiri mambo hayo
kufanywa na Serikali.
Ndugu zangu
watanzania Latifa Saidi anaomba msaada wetu kwa chochote kile atakachosaidiwa
kwake kitakuwa ni kikubwa kwa yeyote atakaye guswa na kutaka kumsaidia ana weza
kuwasiliana naye moja kwa moja kwa namba ya simu 0788034472 au Mwandishi wa
taarifa hii kwa namba 0754362990.
Mtoto Abubakar Tenda (10) anayesumbuliwa na maradhi.
Mtoto Abubakar Tenda (10) akiwa na mama yake.
Mtoto Abubakar Tenda (10) anayesumbuliwa na maradhi akiwa amekaa na mama yake nje ya upenu wa nyumba ya jirani yao anapojishughulisha mama huyo kutengeneza sambusa za viazi mviringo ili aweze kujipatia fedha za kujikimu katika maisha ya kila siku.

No comments:
Post a Comment