ZAINAB SHOMARI:UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHUMI NI UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM. - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Sunday, 25 May 2025

ZAINAB SHOMARI:UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHUMI NI UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM.

MAKAMU Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania (UWT) Ndg. Zainab Khamis Shomari (MNEC) amesema Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia Ilani ya Uchaguzi 2020-2025 ilianisha uwepo uwezeshaji Wananchi kiuchumi kwa dhumuni la kuimarisha uchumi wa mwananchi mmoja mmoja.

Makamu Zainab ametoa wito huo Leo Tarehe 25 Mei, 2025, wakati wa Hafla ya kukabidhi fedha kwa vikundi 211 katika Jimbo la Chaani, Wilaya ya Kaskazini 'A' Kisiwani Unguja.

"Serikali ya awamu ya Nane inayoongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi imekuwa ikitekeleza Ilani ya CCM kwa kishindo katika Sekta mbalimbali ikiwemo uwezeshwaji wananchi kwa kuwapatia rasirilimali mbalimbali ikiwemo fadha taslimu"

"kipekee nitoe pongezi kwa Muwakilishi wa Jimbo la Chaani Mhe. Nadir Abdulatif Yussuf Al-wardy kwa kuandaa mpango huu wa kuwawezesha Wananchi wa jimbo hili"

Makamu Mwenyekiti Zainab ameongeza kusema kuwa jitihada kubwa zinatakia kuendelezwa ili kuwahimiza wanawake kushiriki kikamilifu Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Mwezi Oktoba, 2025 kwa kuwachagua Viongozi wanaotokana na Chama Cha Mapinduzi ili waendelee kuwaletea maendeleo Mbalimbali katika Maeneo yao.

No comments:

Post a Comment