KASEKENYA AWATAKA VIJANA ILEJE KUJIKITA KWENYE MICHEZO - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Tuesday 15 October 2024

KASEKENYA AWATAKA VIJANA ILEJE KUJIKITA KWENYE MICHEZO

Naibu Waziri wa Ujenzi na Mbunge wa Jimbo la Ileje, Mhandisi Godfrey Kasekenya akizungumza na wananchi wa kijiji cha Sange, wilayani Ileje, mkoani Songwe alipokuwa akizundua ligi ya Kasekenya Cup jimboni humo.

Naibu Waziri wa Ujenzi na Mbunge wa Jimbo la Ileje, Mhandisi Godfrey Kasekenya akipokea zawadi ya mipira kutoka kwa Afisa michezo wa wilaya ya Ileje mkoani Songwe alipokuwa akizundua ligi ya Kasekenya Cup jimboni humo.

NAIBU Waziri wa Ujenzi na Mbunge wa Ileje, Mhandisi, Godfrey Kasekenya amewataka vijana Wilayani Ileje, mkoani Songwe kujikita kwenye michezo na kutumia fursa ya mashindano ya kombe la Kasekenya kuimarisha afya, ushirikiano na kukuza vipaji.

Akizindua Bonanza la kuhamasisha michezo Wilayani huko, Mbunge Kasekenya amesema wilaya hiyo imedhamiria kuwekeza kwenye michezo ili kukuza vipaji vya vijana na kuwawezesha kupata ajira.

"Mashindano haya yatumike kama chachu ya kuhamasishana kufanya kazi kwa bidii na kukuza vipaji kwani michezo ni ajira, afya na urafiki", amesema Mhandisi, Kasekenya.


Aidha, Kasekenya amesema kuwa Mashindano hayo pamoja na mambo mengine yanahamasisha wananchi kujiandikisha kupiga kura, kugombea na kushiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa Novemba 27 mwaka huu.


Amefafanua kuwa Bonanza hilo ambalo ni uzinduzi wa Kasekenya Cup limekutanisha timu za mpira wa miguu wanaume na wanawake, vikundi vya muziki wa asili, riadha, na uchezaji wa muziki ambapo washindi wamejizolea zawadi mbalimbali.


Katika soka, timu ya Makaburu ya jimbo la Busokelo, mkoani Mbeya imeifunga kombaini ya Sange iliyopo wilayani Ileje, mkoani Songwe bao 3 kwa 2 wakati wanawake Lubanda wakishinda kwa penati 3 kwa 2 dhidi ya Kalembo FC baada ya sare ya bao 2 kwa 2.


Viongozi mbalimbali wa Kata, Tarafa, Wilaya na Mkoa wa Songwe wa vyama na Serikali wameshiriki Bonanza hilo.

No comments:

Post a Comment