DKT. NCHEMBA AMWAKILISHA RAIS SAMIA MKUTANO WA AFRIKA50 MADAGASCAR - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Friday 20 September 2024

DKT. NCHEMBA AMWAKILISHA RAIS SAMIA MKUTANO WA AFRIKA50 MADAGASCAR

Waziri wa Fedha. Mhe Dkt. Mwigulu Lamewck Nchemba Madelu (Mb) (kushoto) akiwa na Rais wa Madagascar, Mhe. Andry Rojaelina (katikati) na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Taasisi ya Africa50, ambaye pia ni Rais wa Benki ya Maendeleo ya Africa (AfDB), Dkt. Akwinumi Adesina baada ya Rais huyo kufungua rasmi  Mkutano wa Mwaka wa Wanahisa wa Taasisi ya Africa50 na Jukwaa la Miundombinu la Afrika Taasisi ambayo Tanzania ni mwanachama, katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Ivato, mjini Antananarivo nchini Madagascar. Mkutano ulioangazia masuala ya ujenzi na ufadhili wa miundombinu pamoja na matumizi ya nishati safi ya kupikia. Mhe. Dkt. Nchemba, alipomwakilisha Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Mkutano huo (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha, Antananarivo, Madagascar.

Na Benny Mwaipaja, Antananarivo

WAZIRI wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), ametoa wito kwa nchi za Afrika kutafuta njia na mikakati ya kuboresha uchumi na maisha ya wananchi wake kwa kutumia nishati safi ya kupikia ikiwa ni hatua pia ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya Tabianchi yanayochangiwa na uharibifu wa mazingira.

Dkt. Nchemba ametoa wito huo, katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Ivato, mjini Antananarivo nchini Madagascar, kwa niaba ya Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati akihutubia katika Mkutano wa Mwaka wa Wanahisa wa Taasisi ya Africa50 na Jukwaa la Miundombinu la Afrika Taasisi ambayo Tanzania ni mwanachama, na kufunguliwa na Rais wa Nchi hiyo, Mhe. Andry Rajoelina.

Aidha, Dkt. Nchemba alizishauri nchi hizo kuwekeza katika kutoa elimu kwa umma kuhusu umuhimu wa wananchi wao kutumia nishati safi ya kupikia pamoja na faida zinazoambatana na utunzaji wa mazingira kiuchumi na kijamii.

Dkt. Nchemba pia ametoa wito kwa taasisi za fedha na sekta binafsi kushiriki katika kampeni ya matumizi ya nishati safi ya kupikia ikiwemo gesi iliyosindwa, nishati ya jua, umeme wa joto ardhi, biogas, kwa kuwezesha upatikanaji wa fedha na pia kuzalisha vifaa ama majiko yanayotumia nishati hiyo.

Akifungua Mkutano hup wa Wanahisa, Rais wa Madagascar, Mhe. Andry Rajoelina, alisema kuwa nchi za Afrika hazinabudi kuunganisha nguvu na kutafuta muafaka wa matatizo ya kiuchumi na umasikini unaowakabili wananchi wake.

Alisema kuwa matumizi sahihi ya nishati ya kupikia sit u kwamba yatachangia kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi, bali pia yatakuza ajira na kuboresha maisha ya wananchi.

Nchi yake inapiga hatua kimaendeleo lakini inakwamishwa na matumizi mwakubwa ya fedha kugharamia nishati ya umeme.

Katika msafara huo, Mhe. Dkt. Nchemba ameambatana na Naibu Katibu Mkuu anayesimamia Fedha za Umma (Public Finance Management) Bi. Amina Khamis Shaaban na Balozi wa Tanzania nchini Madagascar, Mhe. Faustine Kasike.

Mkutano wa Wanahisa wa Africa50, umewakutanisha wadau mbalimbali kutoka Bara la Afrika na duniani kwa ujumla wakiwemo Wawekezaji kutoka Taasisi za Umma na Sekta Binafsi, wakopeshaji, wataalam wa ujenzi wa miundombinu na kuwawezesha kutafuta suluhisho la changamoto za miundombinu katika Bara la Afrika pamoja na kukabikliana na athari za mabadiliko ya tabianchi na kuhimiza  kuhusu matumizi ya nishati safi ya kupikia ili kuchochea uchumi na maendeleo ya nchi hizo.

No comments:

Post a Comment