TFRA YATAKA NISHATI MBADALA INUFAISHE HATA WAKULIMA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya

Sunday, 9 June 2024

TFRA YATAKA NISHATI MBADALA INUFAISHE HATA WAKULIMA

Ofisa Mtendaji Mkuu wa TFRA, Joel Laurent (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari alipokuwa akitembelea mabanda mbalimbali wakati wa hafla ya ufungaji Maadhimisho 15 ya Kitaifa ya Wiki ya Nishati Jadidifu Tanzania. Kulia ni Mwenyekiti wa TAREA, Eng. Prosper Magali akifuatilia.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa TFRA, Joel Laurent (wa pili kushoto) akisisitiza jambo alipokuwa  akitembelea mabanda mbalimbali wakati wa hafla ya ufungaji Maadhimisho 15 ya Kitaifa ya Wiki ya Nishati Jadidifu Tanzania.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa TFRA, Joel Laurent (wa pili kushoto) akipewa maelezo toka Banda la REA alipokuwa akitembelea mabanda mbalimbali wakati wa hafla ya ufungaji Maadhimisho 15 ya Kitaifa ya Wiki ya Nishati Jadidifu Tanzania. Kulia ni Mwenyekiti wa TAREA, Eng. Prosper Magali akifuatilia.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa TFRA, Joel Laurent (wa pili kushoto) akipewa maelezo kutoka kwa washiriki wa maonesho ya Maadhimisho 15 ya Kitaifa ya Wiki ya Nishati Jadidifu Tanzania.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa TFRA, Joel Laurent (wa pili kulia) akipewa maelezo toka mabanda anuai alipokuwa akitembelea mabanda hayo wakati wa hafla ya ufungaji Maadhimisho 15 ya Kitaifa ya Wiki ya Nishati Jadidifu Tanzania.

Mwenyekiti wa TAREA, Eng. Prosper Magali (katikati) akizungumza na waandishi wa habari alipokuwa akitembelea mabanda mbalimbali wakati wa hafla ya ufungaji Maadhimisho 15 ya Kitaifa ya Wiki ya Nishati Jadidifu Tanzania.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa TFRA, Joel Laurent (kushoto) akisaini kitabu cha wageni alipotembelea Banda la Kampuni ya Sun King-Tanzania wakati wa hafla ya ufungaji Maadhimisho 15 ya Kitaifa ya Wiki ya Nishati Jadidifu Tanzania. 

Katibu Mtendaji wa TAREA, Eng. Mathew Matimbwi akizungumza kwenye hafla ya ufungaji Maadhimisho 15 ya Kitaifa ya Wiki ya Nishati Jadidifu Tanzania.

MAMLAKA ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) wadau wa nishati jadidifu Tanzania kupeleka huduma zao vijijini ili kuwezesha maendeleo ya kilimo na kunufaisha wakulima na wakazi wa vijijini.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa TFRA, Joel Laurent alisema hayo jana wakati akifunga Maadhimisho 15 ya Kitaofa ya Wiki ya Kitaifa ya Nishati Jadidifu Tanzania akisisitiza kuwa, kuna uhusiano mkubwa kati ya nishati jadidifu na maendeleo ya kilimo.

Katika maadhimisho hayo yaliyomalizika juzi Dar es Salaam, Laurent aliyemwakilisha Waziri wa Kilimo, Hussein bashe alisema: “Kuna uhusiano mkubwa na wa moja kwa moja kati ya nishati mbadala na kilimo kwa kuwa inaweza kumfikia mkulima kwa karibu na kwa gharama nafuu kwa ajili ya utumiaji mitambo ikiwamo ya kumwagilia mashamba na maendeleo ya kilimo katika kuongeza tija na kukuza uchumi.”

Alisema changamoto iliyopo ni kuhakikisha masuala yote yanayokwamisha upatikanaji, kuenea na kuongezeka kwa matumizi ya nishati jadidifu kwa wananchi wote vijijini na mijini zinashughulikiwa ipasavyo.

“Nawashauri muwe tayari kupeleka huduma zenu vijijini ili kuwezesha kilimo mahiri. Mkitekeleza ushauri wangu, mnyororo wa kilimo utaimarika na hivyo kuongeza uzalishaji na mapato… Mkitekeleza ushauri wangu, mnyororo wa kilimo utaimarika na hivyo kuongeza uzalishaji na mapato,” alisema Laurent.

Alisema Serikali imeanzisha taasisi mbalimbali ikiwamo Tume ya Taifa ya Umwagiliaji na miradi ya kimkakati ya kilimo yenye fursa kubwa kutumia nishati mbadala katika mnyororo wa kilimo kwani kuna uhusiano mkubwa kati ya kilimo na nishati jadidifu.

“Mafanikio katika sekta zote za uchumi, huduma za jamii na maendeleo yanategemea kwa kiasi fulani upatikanaji wa uhakika na endelevu wa nishati ya kutosha ambayo haina madhara,” alisema.

Meneja Mafunzo wa Sun King- Tanzania ambao ni wafadhili wakuu, Immaculate Shija alisema kilichoisukuma kampuni hiyo kufadhili maadhimisho ya mwaka huu, ni namna maadhimisho yaliyopita kutokuwa na nguvu kubwa, licha ya kuwa ni muhimu katika kuunga mkono juhudiza serikali kutunza mazingira na afya za watu kupitia matumizi nishati safi.

“Tumesukumwa na ujumbe mkubwa uliokuwa ukitolewa kupitia maadhimisho haya na tunatathmini kuona penye changamoto, tulipofanya vizur na hatakwa watunga sera kuona sehemu na namna ya kuboresha.

Mwenyekiti wa TAREA, Eng. Prosper Magali alisisitiza kuwa TAREA inasimama katika kuunga mkono azma inayoendelea ya kuwezesha upishi safi kupitia uhamasishaji wa matumizi ya teknolojia ya nishati mbadala kwa kupikia ambayo itachangia uhifadhi wa misitu ya Tanzania, kuboresha utunzaji wa mazingira na kupunguza ongezeko la hewa ukaa nchini.

Magali alisema kuwa TAREA na wadau wa nishati jadidifu wamedhamiria kuhakikisha kuwa teknolojia ya nishati jadidifu inafika maeneo mbalimbali nchini licha ya changamoto ya fedha iliyopo.

Awali, Katibu Mtendaji wa TAREA, Eng. Mathew Matimbwi alikaribisha ufunguzi rasmi kwa kuitaka Wizara ya Nishati kufikiria kupitia upya Sera ya Nishati ili kuwezesha kutilia mkazo matumizi ya nishati mbadala kwa aina zote za maombi badala ya kuzingatia uzalishaji wa umeme pekee. Pia aliiomba Wizara kuishauri Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kuteua mwakilishi wa sekta binafsi katika Bodi ya REA kutoka kwa wadau wa nishati.

Matimbwi alisema TAREA inaunga mkono azma inayoendelea ya kuwezesha upishi safi kupitia uhamasishaji wa matumizi ya teknolojia ya nishati mbadala kwa kupikia ambayo itachangia uhifadhi wa misitu ya Tanzania, kuboresha utunzaji wa mazingira na kupunguza ongezeko la hewa ukaa nchini huku akisistiza kuwa,  kuna uhusiano mkubwa kati ya maendeleo ya teknolojia ya nishati mbadala na ulinzi wa mazingira.

Katika hafla hiyo ya ufungaji, Matimbwi aliiomba Wizara ya Kilimo na Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kuingiza teknolojia ya nishati jadidifu katika mnyororo wa thamani wa kilimo na kuishukuru serikali kwa jitihada zake za kuandaa mpango mkuu wa umwagiliaji unaoweza kutumia nishati jadidifu kama vile umwagiliaji wa jua.

Mwenyekiti wa TAREA, Eng. Prosper Magali alisisitiza kuwa TAREA na wadau wa nishati jadidifu wamedhamiria kuhakikisha teknolojia ya nishati jadidifu inafika maeneo mbalimbali nchini licha ya changamoto ya fedha iliyopo.

TFRA yataka nishati mbadala inufaishe hata wakulima

No comments:

Post a Comment