Na Adeladius Makwega - MWANZA
CHUO Cha Maendeleo ya Michezo Malya (MCSD) kimefanya uchaguzi wa viongozi wa Serikali ya Wanachuo Juni 7, 2024 na kumchagua George Mkinga kuwa Rais wa Serikali ya Wanachuo.
Uchaguzi huo ulianza kwa kila mgombea wa kila nafasi kujinadi na kutolewa nafasi ya kila mgombea kuulizwa maswali matatu lakini mgombea George Mkinga pekee ndiye aliyeulizwa maswali katika mkutano huo wa uchaguzi.
Jambo hilo lilistajabisha wengi lakini ndivyo hali ilivyokuwa, huku wapiga kura wakishangilia kwa shangwe tele.
Mara baada ya maswali hayo kura zilipigwa na kuhesabiwa, lilipokamilika zoezi hilo lilmuamsha katika kiti chake Mwadili Wa Wanachuo Bi Epifania Bugaga na kuyasoma matokeo yote.
“Kwa Nafasi ya Katibu Serikali ya Wanachuo Hamis Maleka alipata kura 82 naye Francis Maramonyi alipata kura 141. Kwa nafasi ya Makamu wa Rais Serikali ya Wanachuo Mayasa Semtibua alipata kura 82 naye Costansia Kisega alipata kura 141 na kwa nafasi ya Urais Abdalah Msabaha alipata kura 79 naye George Mkinga alipata kura 145 huku jumla ya kura zote ni 231 nazo kura chache kuharibika.”
Kulingana na matokeo hayo Costansia Kisega alichaguliwa Makamu wa Rais naye Francis Maramonyi alichaguliwa Katibu Serikali ya Wanachuo.
Akizungumza mara baada ya ushindi huo ndugu George Mkinga amesema kuwa uchaguzi umekwisha sasa ni wakati wa kuwajibika kilamoja atimize majukumu yake pahala atakapapongiwa na pahala alipo.
No comments:
Post a Comment