Naibu Waziri Mkuu na Waziri Nishati, Dk Doto Biteko.
TANZANIA RENEWABLE ENERGY ASSOCIATION (TAREA)
TANGAZO
Maonesho Wiki ya
Nishati Jadidifu, JUNI 6-7, 2024
Jumuiya ya Wadau wa
Nishati Jadidifu Tanzania (TAREA), kwa kushirikiana na Wizara ya Nishati kwa
udhamani mkuu wa Sunking, inawaalika Wananchi wote katika Maonesho ya Kitaifa
ya Nishati Jadidifu (Renewable Energy) yatakayofunguliwa
Alhamisi Juni 6 na Naibu Waziri Mkuu na Waziri Nishati, Dk Doto Biteko na
kufungwa na Waziri wa Kilimo, Husein Bashe Ijumaa, Juni 7, mwaka huu.
Kaulimbiu ya Mwaka huu
ni: NISHATI JADIDIFU KWA UCHUMI SHIRIKISHI NA WA KIJANI (RENEWABLE ENERGY FOR
INCLUSIVE AND GREEN ECONOMY)
Wiki ya Nishati
Jadidifu itakuwa na maonesho yanayohusisha Umeme wa Jua yaani Sola, Upepo,
Joto-ardhi na majiko banifu sambamba na warsha yenye mada mbalimbali kuhusu
nishati jadidifu.
Wadau wa maendeleo,
kampuni na taasisi binafsi na serikari watakuwa katika mabanda kutoa elimu na
kuuza bidhaa mbalimbali za nishati jadidifu kutoka kwa wataalamu waliobebea.
Wadhamini wengine wa
Maonesho hayo yatakayofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius
Nyerere Posta, Dar es Salaam ni Jumuiya ya Umoja wa Ulaya (EU), Expertise
France, Ensol, GOGLA, Tanesco, Wakala wa Nishati Vijijini (REA), AECF na UNDP
HAKUNA KIINGILIO.
WOTE MNAKARIBISHWA.
Kwa taarifa zaidi piga
0765 098 462.
Tanzania Renewable
Energy Association(TAREA)
Plot 1080, Mandela
Road, Mabibo External,
Export Processing Zone Authority
Shopping Arcade 17,
P.O. Box 32643,16106
Dar es Salaam, Tanzania.
No comments:
Post a Comment